Home Michezo ZIGO LA EURO NA Hisense , KUANZA SAFARI YA UJERUMANI KESHO, SOMA...

ZIGO LA EURO NA Hisense , KUANZA SAFARI YA UJERUMANI KESHO, SOMA HAPA KUWA MIONGONI MWAO

 .

Aileen Kokushibila Tinka Mkazi wa Dar es Salaam ( Kulia ) ambaye ni mshindi wa tiketi ( Wiki ya Tano ) Kampeni ya ZIGO la EURO CUP na Hisense, safari iliyolipiwa kila kitu  kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora, akikabidhiwa Mfano wa Tiketi tukio lililofanyika mapema leo hii June , 28 , 2024 Makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es Salaam , Bi. Aileen ameibuka mshindi baada ya kubashiri Mechi na PariMatch kupitia Tigo Pesa Super App, katikati ni Meneja Biashara Tigo Pesa Bw. Fabian Felician na Mwakilishi wa Hisense Joseph Mavula , Kushoto ni Balozi wa PARIMATCH Mchekeshaji Kiredio.

Na Adery Masta.

Aileen Tinka Mkazi wa Dar Es Salaam, ni Mteja wa Tigo wa Tano kujishindia Safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda kutazama Mechi za Kombe la EURO 2024 , ambapo timu 24 zinatarajiwa kuchuana katika miji 10 mwenyeji Nchini Ujerumani . 

Aileen  ameshinda kupitia Kampeni ya ZIGO LA EURO CUP NA Hisense , iliyozinduliwa wiki kadhaa Zilizopita ambapo Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO, kwa kushirikiana na Parimatch na Hisense waliileta kusambaza Tabasamu kwa Wateja wao , Ikumbukwe Ailleen ni Mshindi wa Wiki ya Tano akitanguliwa na Aida Juma Mshindi wa Wiki ya Tatu,  Ramadhan Mrutu Mshindi wa Wiki ya Kwanza , Emmanuel Mlonjela Mshindi wa Wiki ya Pili  na William Mshery Mshindi wa wiki ya nne , Ikumbukwe ndani ya Wiki tano  sasa Tigo , PariMatch na Hisense wameshatoa zawadi za Vifaa vya Hisense ( TV na Friji ) , Pesa Taslimu, na Tiketi za Kushuhudia EURO kwa Watanzania zaidi ya 28.

Washindi ( watatu kati ya hao ) wa Kifurushi cha HISENSE wiki ya Tano kampeni ya ZIGO LA EURO na Hisense  ambacho ni TV na Friji katika picha ya pamoja muda mchache baada ya kukabidhiwa zawadi zao .Ili kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia tiketi au zawadi ya fedha taslimu TZS 1,000,000, na Vifaa vya Hisense TV na Friji washiriki wanapaswa kujiandikisha na Parimatch, kuweka pesa zao kupitia Tigo Pesa kisha kuweka dau ( betting ) kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu na Parimatch. Kadiri dau zinavyowekwa, ndivyo nafasi zinavyoongezeka ya kushinda TZS 1,000,000 au tiketi ya safari na mechi yenye malipo kamili ya kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!