> Ndege mpya za KLM Royal Dutch ambazo ni AIRBUS A321neo na AIRBUS A320neo zitachukua nafasi ya ndege ya kizamani ya BOEING 737s kwa safari za Ulaya.
Na Adery Masta
Septemba 9, 2024 Nairobi Nchini Kenya , Shirika la Ndege la KLM Royal Dutch limetangaza ujio wa Ndege aina ya AIRBUS A321neo , ambayo inaenda kuchukua nafasi ya BOEING 737 lengo kubwa likiwa ni kuwahakikishia Wateja wao safari salama na yenye utulivu huku likitunza mazingira.
Ndege hii mpya ina Injini mpya inayozalisha kiwango kidogo cha hewa ya Carbon dioxide ( Co2 ) ukilinganisha na ndege nyingine zilizopita , huku ikizingatia usalama zaidi, na kumwondelea usumbufu Mteja hasa ule unaotakana na Mafuta pamoja na kelele muda wote wa safari.
Akizungumza katika utambulisho wa Ndege hii mpya na ya kisasa , Rais na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa KLM Bwn. Marjan Rintel amesema .
Kwa muda mrefu shirika hilo linatazamia kuendelea kufanya mapinduzi makubwa katika SEKTA ya Usafiri wa Anga kwahiyo ujio wa A321 neo ni ushahidi tosha kwamba wamedhamiria kuziondoa Ndege zao za Boeing 737 ili kuleta Ndege nyingine mpya na za kisasa zenye Ubora wa hali ya juu.
Tafadhari tembelea mitandao Yao ya kijamii kwa taarifa zaidi kuhusiana na mapinduzi haya makubwa yaliyofanywa na Shirika la KLM katika safari zao za Anga.