Home Biashara ZIARA YA RAIS SAMIA AFRIKA KUSINI YALETA MATOKEO CHANYA SEKTA YA MADINI

ZIARA YA RAIS SAMIA AFRIKA KUSINI YALETA MATOKEO CHANYA SEKTA YA MADINI

Zaidi ya wawekezaji 30 kutoka Afrika Kusini wameingia nchini

Wamepongeza marekebisho ya Sheria yaliyofanyika sekta ya Madini

Baada ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya hivi karibuni nchini Afrika Kusini, ujumbe wa Wawekezaji zaidi ya 30 kutoka nchi hiyo wamekutana na Wizara ya Madini pamoja na Taasisi zake kwa lengo la kupata uelewa wa mazingira ya uwekezaji nchini.

Katika kikao kilichowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Madini pamoja na Taasisi zake, Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga amewashauri wawekezaji hao kuwekeza kwenye shughuli za Madini ikiwemo Uchimbaji wa Madini, Uongezaji Thamani Madini na uuzaji wa vifaa vya shughuli za madini.

Akiwasilisha mada kwa wawekezaji hao, Dkt. Mwanga amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na Madini ya aina mbalimbali yakiwemo Madini ya kimkakati ambayo kwa sasa dunia inayahitaji kwa kiwango kikubwa kwa ajili ya maendeleo ya teknolojia ambapo amewakaribisha kuwekeza nchini ili pande zote ziweze kunufaika na uwepo wa Madini hayo.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mwanga amewapongeza wawekezaji hao kwa kufika nchini ili kupata maelezo na kujifunza mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania na amewaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha shughuli za uwekezaji nchini.

Pia, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetumia fursa hiyo kuwasilisha mada juu ya uwepo wa Madini na kiwango cha Madini kilichopo katika maeneo mbalimbali ya nchi pamoja na jiografia ya Tanzania.

Katika hatua nyingine, Afisa Masoko Mark Stephano kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) amewasilisha mada kwa wawekezaji hao ambapo amesema shirika hilo lipo tayari kuungana na mwekezaji yeyote kutoka ndani au nje ya nchi ili kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kunufaisha pande zote mbili.

Kwa upande wake, kiongozi wa ujumbe huo Roelof Tonder amesema Afrika Kusini imeanza shughuli za Madini miaka mingi iliyopita hivyo, imefarijika kuona Tanzania imefanya marekebisho makubwa kwenye Sheria ya Madini ambayo yanalenga kuinufaisha nchi pamoja na Wananchi.

Tonder amesema ujumbe uliyofika nchini Tanzania unatamani kuwekeza katika maeneo tofauti hususan kwenye sekta ya Madini ambapo amesema Ujumbe umefurahishwa na hali nzuri ya utulivu wa Kisiasa uliyopo nchini humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!