Baraza la Mchele Tanzania RCT wameomba Serikali’ na Wadau wa elimu nchini wawekeze kwenye tafiiti ndogo ndogo za zao la mpungai kuanzia elimu ya Sekondari hadi vyuo vikuu ili kurisisha ujuzi na uzoefu wa kuendeleza kilimo cha mpunga nchini.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mchele Tanzania RCT Geoffrey Rwiza kwenye mkutano wa Jukwaa la Wadau wa Mchele Wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Amesema Wanafunzi shuleni hufanya miradi maalumu ya tafiiti za kimafunzo kwa Wanafunzi kwa lengo la kuwajengea uwezo wapate ujuzi ili waendeleze kilimo cha mpunga nchini hapo baadae.
Rwiza alisema Wanafunzi waelekezwe kufanyia tafiiti zao hilo la mpunga ili isaidie kuibua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wakulima wa mpunga nchini.
“Lakini pia kuwatamanisha Wanafunzi kuwa na hamu na kiu ya kuhudumia sekta ya Mchele”Waje huku nako wafanye tafiiti wakiwa kidato cha nne ili wakifika kidato cha tano na sita hadi kikuu wawe na uelewa mkubwa wa zao la mpunga”
“Waipende sekta ya kilimo cha mpunga kwa kuwa watakuwa wamefanyia tafiiti hapo awali kwa muda mrefu” alisema Rwiza.