Zaidi ya asilimia 75% za Makampuni zimekuwa zikifanya makosa madogo madogo katika Uwasilishaji wa taarifa za Umiliki Manufaa katika sehemu mbalimbali kama vile Ukokotoaji wa hisa na uwasilishaji wa Umiliki Manufaa na kumtambua Mmiliki manufaa baada ya kuchukuliwa sampuli za takwimu ya taarifa elfu kumi na tano (15000) zilizowasilishwa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Usajili wa Makampuni na majina ya Biashara (Brela) Mr.Isdor Nkindi katika mwendelezo wao wa kuendelea kuwajengewa uwezo Mabenki na Wanasheria leo Machi 14, 2024 jiji Dar es salaam
Aidha Nkindi amesema uwasilishaji wa taarifa hiyo toka Mwaka 1921 yalipoanza rasmi matumizi ya mfumo na kutekelezwa kwa Sheria ya Umiliki Manufaa “Tathmini yetu imeonesha kwamba kumetokea mapungufu kadhaa yanayotokana na uelewa wa dhana yenyewe lakini pia wale ambao wanaotakiwa wawasilishe hizo taarifa kutoelewa mipaka ya uwasilishaji, baada ya kufanya iyo tathmini tukaona ni muhimu kuendelea kuwajengea uwezo pale ambapo wamekwama“
Hata hivyo Nkindi amesema baada ya kutambua makosa hayo wametoa Elimu na msaada juu ya Umiliki Manufaa kwa kutekeleza Azimio la Kimataifa No.24 ili kujua nani Mmiliki na nyuma ya huyo Mmiliki ni nani ananufaika na bidhaa hiyo hivyo wanatarajia baada ya mafunzo hayo itapunguza kukua kwa kasi ongezeko la makosa ya Kifedha.
Kwa upande wake Jaji Mstaafu wa Mahakama kuu, Jaji Robert Makalamba ameeleza kuwa lengo kubwa ni kuwaelimisha watu watambue haki zao na kufuata Sheria na sio kutafuta wahalifu hivyo ni muhimu kutambua Mmiliki halisi wa Kampuni ambaye anapata manufaa kwa kinachowekezwa katika kampuni hiyo na kama kuna makosa yanayotendeka basi yaweze kutatulia isipokua makosa yanayofanywa kwa makusudi.
Vilevile mmoja kati ya waliopata Elimu hiyo Grace Mutani kutoka kampuni ya Bowman’s Limited Tanzania ameeleza kuwa amejifunza vitu mbalimbali ikiwemo dhana nzima ya Umiliki Manufaa na kufahamu kuwa Mmiliki Manufaa lazima awe na Umiliki wa Asilimia zaidi ya 5% katika kampuni ,Uwezo wa kufanya maamuzi, na pia awe na uwezo wakuendesha Kampuni na kushauri pia upo umuhimu wa Wamiliki kujua na kufuata Sheria ili kuleta uwazi na Manufaa katika kampuni.