Home Michezo YANGA TAWI LA MARA NA BENKI YA NMB WATOA SADAKA KWA WATOTO...

YANGA TAWI LA MARA NA BENKI YA NMB WATOA SADAKA KWA WATOTO WENYE UHITAJI

Na Shomari Binda-Musoma

VIONGOZI, wanachama na mashabiki wa timu ya Yanga tawi la Mara kwa kushirikiana na benki ya NMB wametoa sadaka ya vitu mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji.

Sadaka hizo zimetolewa kwenye shule ya msingi Mwisenge B yenye watoto wenye uhitaji maalumu wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi na wasioona.

Mwenyekiti wa Yanga tawi la Mara Ismail Massero amesema katika kilele cha wiki ya wananchi wameamua kuwafikia watoto hao.

Amesema maelekezo ya viongozi wa taifs ni kuhakikisha mikoa yote inashiriki kwa pamoja kufika kwa jamii na kutoa misaada mbalimbali.

Massero amesema katika kutoa kwa jamii wamrwafikia watoto wa shule ya msingi Mwisenge na kutoa sadaka ya sukari,sabuni,juice,maji na mahitaji mengine kwa kushirikiana na benki ya NMB.

Tunaishukuru benki ya NMB kwa kushirikiana nasi katika kilele cha siku ya mwananchi na kuwatembelea watoto na baadae tutaenda kupata elimu namna ya kupata kadi za uanachama na mashabiki” amesema Massero.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwisenge, agawa Thomas amewashukuru wana Yanga na benki ya NMB kwa kuwafikia na kutoa sadaka kwa watoto.

Meneja wa benki ya NMB tawi la Musoma,Sospetet Justin,amesema watashirikiana vyema na timu ya Yanga kuhakikishs kila mmoja anapata kadi yake..

Amesema maafisa wa benki ya NMB tawi la Musoma wapi tayari kwa kuwahudumia wana Yanga wote na kila mmoja kupata kadi yake ikiwa ya uanachama na mashabiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!