Home Michezo YANGA TAWI LA MARA LAHIMIZA MASHABIKI KUWA WANACHAMA

YANGA TAWI LA MARA LAHIMIZA MASHABIKI KUWA WANACHAMA

Na Shomari Binda-Musoma

MWENYEKITI wa Yanga tawi la Mara, Ismail Massaro, amewataka mashabiki wa timu hiyo kubadilika na kuwa wanachama kamili.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa wanachama uliohudhuliwa pamoja na mashabiki amesema kuwa mwanachama ndio kuisaidia timu.

Amesema utaratibu wa kuwa mwanachama kwa sasa ni rahisi kwa kutumia simu ya mkononi ambapo kila mmoja anaweza kujisajili.

Massaro amesema tawi la Yanga mkoa wa Mara kwa sasa lina wanachama 130 ambao wamejisajili ambao wanapaswa kuongezeka.

“Leo tuna mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho lakini tumekutana pia kwenye mkutano mkuu wa kawaida ili kujadili masuala.mbalimbali ya timu na tawi letu.”

Kubwa ni kuwaomba wale mashabiki ambao bado hawajajisajili kuwa wanachama wafanye hivyo ili tuweze kwenda pamoja”, amesema Massaro.

Amesema tawi la Mara lina maendeleo mazuri na viongozi wanafanya kazi nzuri ya ushirikishaji baina ya viongozi na wanachama.

Akizungumzia matokeo ya timu hiyo ya mkondo wa kwanza wa fainali ya kombe la shirikisho kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya US-Algers,amesema bado nafasi ipo kwenye mchezo wa marudiano.

Mhasibu wa tawi hilo, Deusdedith Manase amesema wameanza utaratibu wa kusaidiana kwenye shida na raha hivyo wanachama zaidi wanapaswa kujisajili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!