Home Kitaifa WIZARA YA MAJI NA AFYA KUSHIRIKIANA KUEPUSHA CHANGAMOTO YA MAJI HOSPITALI YA...

WIZARA YA MAJI NA AFYA KUSHIRIKIANA KUEPUSHA CHANGAMOTO YA MAJI HOSPITALI YA MUHIMBILI

Dar es Salaam, 06 Novemba 2022

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso leo ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kuhakikisha huduma za maji ndani ya hospitali hiyo zinaendelea kuwepo.

Katika ziara hiyo Waziri Aweso ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Antony Sanga.

Waziri Aweso ameagiza DAWASCO ihakikishe inapeleka maji ya uhakika kwa sasa na kusaidia uwekaji wa maji ya akiba kama tahadhari kwa baadae.

Akitoa taarifa ya upatikanaji wa maji katika hospitalini hapo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi alieleza umuhimu wa kuwa na akiba ya maji ndani ya Hospitali zote nchini ili kuepusha usumbufu wowote kwa huduma za tiba kwa Wananchi.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Janab Mohamad amefafanua kuwa Hospitali inahitaji angalau akiba ya lita milloni sita (6 ).

Amesema kwa sasa ni vema kitengo cha uchujaji damu (Dialysis) kihakikishiwe uwepo wa maji safi kila siku .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!