Home Kitaifa WIZARA YA UWEKEZAJI KUANZISHA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA HUDUMA ZA PAMOJA KWA...

WIZARA YA UWEKEZAJI KUANZISHA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA HUDUMA ZA PAMOJA KWA WAWEKEZAJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi ameipongea  Wizara ya Uwekezaji na Biashara kwa kuanzisha Mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji  na programu ya utengenezaji wa mashine mbalimbali zinazowezesha uanzishaji wa viwanda .

Rais Mwinyi ameyasema hayo Julai 04 2022 alipotembelea Banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara nakujionea Mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji  na mashine mbalimbali zinazoweza kutumika kuanzisha kiwanda kuanzia milioni sita hadi milioni 600.

Rais Mwinyi amesema hii ni hatua nzuri kwani hata nchi zilizoendelea zilianza kutengeneza mashine kama hizi na sasa zinatengeneza mashine na mitambo mikubwa. Natumaini mwakani mtakuwa na maendeleo makubwa ya mashine hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!