Na Mercy Maimu
Wizara ya Tamaduni, Sanaa na michezo imeahidi kuja na mambo matatu makubwa ya kihistoria katika sekta hiyo Kwa mwaka 2023.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wizara ya Tamaduni Sanaa na michezo Dakta HASSAN ABBASI amesema kuwa mambo yatakayozinduliwa ni Mdundo wa Taifa,Vazi la Taifa na utoaji wa mikopo kwa wasanii,ambapo mambo hayo yatazinduliwa kesho 03/02/2023 Jijini Dar es Salaam.
Dakta Abbasi amesema kuwa Mdundo wa Taifa utajumuisha vionjo kutoka midundo ya makabila mbalimbali nchini ili wasanii wasitoke njee ya muongozo.
Katika hatua nyingine ameipongeza kamati ya kuandaa mdundo wa taifa Kwa kuwaza mbele zaidi katika kutengeneza midundo ya sauti ambapo kunabaadhi ya wasanii ambao wamejitokeza kurekodi nyimbo ambazo zitakwenda kwenye hizo ala za taifa.
“Hatuwezi kuwa na mziki unaokwendakwenda tu kwaiyo lazima mziki wetu update muongozo flani,Mziki wa Tanzania upo katika namna nyingi lakini Kuna namna ambayo ukiisikia tusema hii singeri au taarabu ya Tanzania tunaweza na tunaamini hivyo“. amesema Abbas
Aidha Dakta Abbasi ameeleza jambo la mwisho ni kutoa mkopo Kwa awamu ya pili Kwa wadau wa Tamaduni na Sanaa ili waweze kuendeleza kazi zao mkopo ambao thamani yake ni takribani SH Bilioni Moja ambapo mkopo huo utakuwa Haina riba.
Pia ameongeza kuwa mkopo huo utatolewa Kwa wale ambao wametimiza masharti na vigezo na Moja ya unafuu uliopo katika mkopo huo ni kuanza marejesho baada ya miezi mitatu ambo pia atakaye kopa tatakiwa kumaliza mkopo huo ndani ya miaka miwili.