Home Michezo WIZARA YA MADINI YAWEKA MIKAKATI MIPYA KWA KLABU YAKE YA MICHEZO

WIZARA YA MADINI YAWEKA MIKAKATI MIPYA KWA KLABU YAKE YA MICHEZO

Yaibuka na Medali Nne

Medali za Fedha 2, Shaba 1 na Dhahabu 1

Katika kuhakikisha Klabu ya Michezo ya Madini ( Madini Sports Club) inashiriki michezo kwa mafanikio makubwa imebainisha mikakati ya kiufundi itakayo leta matokeo bora katika michezo.

Mikakati hiyo imebainishwa leo Oktoba 17 , 2023 na Naibu Katibu Mkuu Madini Msafiri Mbibo alipomwakilisha Katibu Mkuu Madini katika kikao cha kupokea taarifa ya ushiriki wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI – 2023) jijini Dodoma.

Mbibo amesema kuwa Wizara imefurahishwa na ushindi mlioupata katika mashindano ya SHIMIWI lakini pamoja na ushindi huo Wizara ina mikakati mbalimbali ya kiufundi ikiwemo mpango wa kushiriki michezo mbalimbali katika ngazi ya mkoa na taifa kwa lengo la kuwajengea uwezo wanamichezo wote.

Mbibo aliongeza kuwa Wizara ina mpango wa kuwa na eneo maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi litakalojumuisha michezo yote pamoja na kuwepo na vifaa vyote vya michezo ili wanamichezo wa klabu ya madini waweze kupata uzoefu kabla ya kuingia katika mashindano.

Sambamba na hayo Mbibo amefafanua kuwa katika michezo motisha ni vyenzo muhimu ya ushindi hivyo Wizara itaendelea kutoa motisha kwa wanamichezo wote kwa jinsi itakavyowezekana nia kubwa ni kutoa hamasa kwa wanamichezo.

Awali akitoa taarifa ya ushiriki Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Madini John Issangu amesema kuwa klabu ya madini ilishiriki kwa ushindani mkubwa na kuweza kupata medali nne ikiwamo ya Dhahabu moja, medali za fedha mbili na Shaba moja.

Akielezea juu ya ushindi huo Issangu amesema Medali hizo zilipatikana katika mchezo wa riadha kuanzia Mbio za mita 100 kwa washiriki kuanzia umri wa miaka 55-60 , medali ya fedha ilipatikana katika Mbio za mita 200 , medali ya tatu ambayo ya fedha ilipatikana katika mita 800 na medali katika mita 400.

Mashindano ya SHIMIWI ujumuhisha michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa Pete, kurusha tufe , mbio za baiskeli na michezo ya ndani kama vile Bao ,Draft na Karata.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!