Home Kitaifa WIZARA YA FEDHA YATOA ELIMU YA KURIPOTI MASUALA YA BAJETI KWA WAMILIKI...

WIZARA YA FEDHA YATOA ELIMU YA KURIPOTI MASUALA YA BAJETI KWA WAMILIKI WA KITANDAO YA KIJAMII

Na Asia Singano na Chedaiwe Msuya – WF – Morogoro.

Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya habari imeahidi kufanya kazi kwa pamoja hasa katika kipindi hiki cha Bajeti kuelekea uwasilishwaji wa Bajeti Kuu ya Serikali inayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni hivi karibuni.

Hayo yameelezwa na Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi Salome Kingdom, katika Kongamano la Elimu kwa Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii Nchini yaliyofanyika mjini Morogoro katika ukumbi wa mikutano wa NaneNane. 

Bi. Salome katika kuwasilisha mada yake kuhusu namna bora ya kuripoti taarifa za bajeti alisema Wizara itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na manufaa yanayopatikana kutokana na ukusanyaji mzuri wa kodi hapa nchini.

 ‘’Serikali inaelekeza zaidi kuongeza mikakati ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, hivyo itaendelea kushirikiana na Sekta ya Habari kutoa elimu  kwa wananchi  wasikwepe kulipa kodi‘’ alisema Bi. Salome.

Aidha aliwapongeza wadau katika sekta ya habari kwani wana nafasi kubwa katika kuchochea maendeleo ya uchumi wetu kwa njia ya kuwahamasisha wananchi kutekeleza kwa pamoja malengo ya Taifa.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Fedha , Bw. Benny Mwaipaja, aliwashukuru wadau na wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini kwa kuendelea kufanya kazi bega kwa bega na Wizara  na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo katika kulijenga taifa letu. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!