Na Magrethy Katengu
Serikali Kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Watu imesema itahakilisha Jiji la Dar es salaam linajengwa kwa kufuata Master plan Ili kutoa suluhisho la changamoto zilizopo katika jiji hilo ikiwemo Ujenzi holela foleni hivyo mpango kabambe utakaondaliea utekelezaji wake utaenda sambamba na usimamizi wa uendelezaji miji kwa kuzingatia matumizi yaliyoainishwa.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula leo katika kikao kazi Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaa ikiwemo Wakuu wa Wilaya zote Watendaji Madiwani lengo ni kujadiliana juu ya mpango huo lakini pia zoezi zima la ukwamuaji urasimishaji ardhi na wananchi kupatiwa vipali vya Ujenzi kabla ya kujenga katika jiji hilo.
Waziri Mabula amesesitiza kila mamlaka ya upangaji inao wajibu wa kisheria kuweka mkakati wa kuzuia uendelezaji usiofuata sheria, kanuni na taratibu kuwa bila kufanya hivyo serikali itashindwa kutekeleza mipango iliyowekwa na hivyo kutumia fedha za wananchi vibaya.
Waziri Mabula amesema kumekuwa na migogoro ya Ardhi hivyo kupitia mpango huo itakuwa ni kuwa Dira ya Jiji endelevu, lenye ushindani linalotumia rasilimali zake kiufanisi na kuhifadhi mazingira na unaolenga kukukuza utamaduni na kuhifadhi historia yake ya muda mrefu.
“Mpango umeandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya 2025 iliyofafanuliwa katika Mpango wa Maendeleo wa 2021-22 hadi 2025-26 na unatoa mwongozo katika utoaji wa maamuzi katika matumizi na maendelezo ya Ardhi ili kuhakikisha uendelezaji wenye mpangilio katika ukuaji wa Jiji la Dar es Salaam hadi mwaka 2036.” amesema Waziri
Hata hivyo Waziri Mabula ameongeza kuwa Mpango huo unatoa majibu ya changamoto zinazolikabili Jiji ikiwemo msongamano wa magari, ujenzi holela, uhaba wa huduma za jamii na miundombinu.
‘’Mapendekezo ya Mpango Kabambe huu yamezingatia uongezaji wa fursa za uwekezaji ambao mwisho wa siku utaongeza ajira kupitia miradi mbalimbali iliyopendekezwa” Alibainisha Waziri Angeline Mabula.
Dkt. Mabula alitaja baadhi ya miradi iliyopendekezwa kuwa ni Ujenzi wa viwanda maeneo ya Pugu, Pembamnazi, Kisarawe II na Kimbiji, Ujenzi wa barabara ya mzunguko katika Manispaa za Ilala na Ubungo, Uboreshaji na uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi.
Miradi mingine ni uhifadhi wa maeneo ya kihistoria katikati ya Jiji, Mradi wa maji safi katika eneo la Kimbiji, Ujenzi wa madampo la kisasa katika maeneo ya Kisopwa na Lingato, Ujenzi wa viwanda vidogo vidogo katika baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa urasimishaji.
‘’Hadi sasa urasimishaji makazi nchini umefanyika katika Mitaa 1961 katika halmashauri 164 za Mikoa yote 26. Katika mitaa hiyo jumla ya viwanja 2,338,926 vimebuniwa kupitia michoro ya mipangomiji 7,051’’. Aliongeza Waziri Mabula.
Waziri Mabula pia ameongeza kuwa Suala la upimaji nalo limefanyika kwa kiasi kikubwa ambapo jumla ya viwanja 1,170,639 vimepimwa na kuidhinishwa ambavyo ni sawa na asilimia 50.4 ya viwanja vyote vilivyopangwa.
Kukamilika kwa Mpango Kabambe huu kumekuja wakati muafaka, pamoja na kutumika kama chombo cha kuongoza na kusimamia uendelezaji wa Jiji na kudhibiti ujenzi holela, pia utatoa uhakika kwa wawekezaji katika Jiji hili, utaondoa changamoto mbalimbali zikiwemo za migogoro ya matumizi ya ardhi, ukuaji wa makazi yasiyo rasmi, uharibifu wa miundombinu, uharibifu wa mazingira na kukuza fursa za uwekezaji na kuongeza ajira kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makala amesema ifike mahali migogoro ya Ardhi katika Mkoa huo iishe Makampuni yote yaliyochukua fedha za upimaji na urasimishaji Ardhi yaanze kazi maana wananchi wanalalamika wametoa fedha lakini bado hawajapewa hati miliki ya eneo
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Watu Allan Kijazi amesema Dar es salaam ni Jiji linaloendelea kuongezeka idadi ya watu hivyo kupitia majadiliano hayo kila Mjumbe aliyehudhuria akiondoka atakwenda kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri.