Home Kitaifa WIZARA YA ARDHI KUKUSANYA MAPATO KWA KUTUMIA MITANDAO YA SIMU NA BENKI

WIZARA YA ARDHI KUKUSANYA MAPATO KWA KUTUMIA MITANDAO YA SIMU NA BENKI

Wizara ya ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi imeandaa utaratibu wa kutumia makampuni ya mitandao ya simu pamoja na benki zilizopo nchini ili kurahisisha zoezi la ukusanyaji wa mapato yatokanayo na sekta ya ardhi.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Allan Kijazi wakati akifungua kikao ambacho kimewakutanisha wadau mbalimbali wa ukusanyaji wa mapato ambapo amealika makampuni mengine yenye Nia ya kushirikiana katika wizara hiyo Ili kuwafikia wananchi wote nchini

“Mtandao mkubwa wa benki upo katika maeneo ya mjini hali inayopelekea watu wa vijijini kukosa huduma na kushindwa kulipa Kodi”

Aidha makampuni ya mitandao ya simu pamoja na makampuni ya Benki yameaswa kuandaa utaratibu mbalimbali ya utoaji wa elimu Kwa wananchi hususani maeneo ya vijijini ili kuongeza uelewa juu ya ulipaji Kodi Kwa njia ya kidigitali.


Serikali imefungua akaunti katika benki mbalimbali zilizopo hapa nchini,na benki hizo zinakusanya mapato kwa niaba ya Wizara,na mapato hayo yanawasilishwa kwenye akaunti za serikali. Na katika kutekeleza mradi huu kuna makubaliano ambayo tumefanya na benki tumeona kuna mafanikio makubwa.”

Mhe Kijazi ameongeza kuwa katika kuhakikisha makampuni hayo yanashiriki kikamilifu katika utoaji wa huduma hiyo wizara imeandaa utoaji wa motisha Kwa makampuni yatakayofanya vizuri katika utoaji wa huduma hiyo na elimu Kwa wananchi

Na katika kufanya hivyo serikali kushirikiana na Wizara ya Ardhi itatoa hamasha kwa benki na mitandao ya simu ambayo itakuwa imefanywa vizuri,nadhani hiyo itakuwa njia nzuri ya kukuza mapato ya Nchi.”


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!