Home Kitaifa Wilaya ya Magu yaazimisha Miaka 62 Kwa kupanda Miti na kuendesha Mdahalo

Wilaya ya Magu yaazimisha Miaka 62 Kwa kupanda Miti na kuendesha Mdahalo

Na Neema Kandoro Mwanza

Katibu Tawala wilayani Magu Jubilate Lawuo ameongoza Makundi ya watu mbalimbali wakiwemo wazee, walemavu, Vijana na wanafunzi katika kuendesha Mdahalo wa Miaka 62 ya uhuru na kupanda Miti.

Lawuo amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuendelea kulinda amani iliyopo kwani ndiyo tunu ya Nchi na inasaidia katika kuchochea maendeleo ya nchi na vilevile amewataka vijana kuwekeza na kujituma kwani wao ndo Nguvu kazi ya Nchi.

Aidha ameendelea kusisitiza wananchi kupinga Rushwa, Ukatili wa kijinsia kwa Makundi ya watoto, wanawake na wanaume pindi wanapoona viashiria hivyo watoe Taarifa Kwa Vyombo husika.

Vilevile amewashukuru wananchi wote kwa kuiamini Serikali yao inayoongozwa na Mama Shupavu na Rais Samia Suluhu Hassani.

Akizungumza kwenye Mdahalo huo Mchungaji mkongwe Jakobo mutashi alisema lengo la Mdahalo huo kuwa ilikuwa kutathimini kipindi cha nyuma na sasa akisema kwa sasa hali ya kisiasa ni Nzuri kuliko siku zilizopita.

Aliwataka watu wote kutumia vizuri muda huu kutathimini Yale yaliyofanywa na kuenzi mazuri yaliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere kwa kutunza utulivu wa Taifa letu Ili wananchi waweze kushiriki katika Shughuli za maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!