Home Kitaifa WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA: NIC YAZINDUA MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA: NIC YAZINDUA MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limesisitizwa a kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi ili kusaidia kuongeza wigo wateja na nchi iweze kunufaika pato lake kuongezeka..

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam Msajili wa hazina Bw Mgonya Benedicto wakati akifungua Maadhimisho ya wiki ya wateja na kushuhudia Mkataba wa Huduma kwa wateja hivyo amewataka watumishi wa NIC kufuata ahadi iliyowekwa kwenye mkataba huo na asiwepo mtumishi yeyote wa kutenda kinyume na mkataba huo kwani atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria na Miongozo ya Utumishi wa Umma.

Nisisitize madhumuni ya mkataba huu ni kuboresha uhusiano baina ya Shirika na wateja wake lakini pia ukikusudia kuongeza uelewa kuhusu aina na ubora wa huduma zinazotolewa, haki na wajibu wa mteja na jinsi anavyoweza kuwasiliana na nyie bila kupata vikwazo”amesema Bw Mgonya

Mkataba wa Huduma kwa Mteja ni makubaliano kati yenu watoa huduma na mteja wenu ikiwa ni ahadi ya kutoa huduma bora kwa mteja, mkataba huu unaelekeza na kuainisha viwango vya huduma ambavyo wateja wenu wanatarajia kupata ili kufikia malengo yao”. Amesema

Aidha amesema Ofisi ya Msajili wa Hazina na Serikali kwa ujumla ipo tayari kuwapa ushirikiano mnaostahili ikiwa tu mtaweka bidii katika kazi na kuboresha huduma zaidi ya zilivyo sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Dkt. Elirehema Doriye, amesema Shirika limekuwa likifanya mabadilikko kwenye kuwahudumia wateja ambapo wamekuwa wakiboresha huduma ili kuendana na ushindani ulioko sokoni jambo lililowavutia wateja kununua bidhaa zao za Bima na kuwafanya kuwa na ukuaji wa faida ya zaidi ya asilimia 100 katika miaka minne mfululizo.

Mojawapo ya misingi inayotuongoza NIC yetu ni dhima kutambua kuwa siku zote “Mteja Kwanza” yaani “Customer first” hii inamaanisha kwamba mteja kwetu ni kipaumbele namba moja katika utoaji huduma”. Amesema Dkt.Doriye.

Aidha Dkt.Doriye amesema katika kuadhimisha wiki hii na kufanya tukio hilo ni kutambua umuhimu wa wateja hivyo Shirika limezindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja “ikiwa ni ahadi yetu kwa wateja kuwa tutawapatia huduma inayostahili kulingana na ahadi tuliyowapa”. Amesema

Nao Miongoni mwa wateja walioalikwa katika hafla hiyo akiwemo Dominata Meena amesema ni jambo la pekee wiki hii ya maadhisho kufanyika kwa kuwaalika kwa kukaa meza moja kubadilisha na mawazo ili taifa lipige hatu ya juu kabisa kiuchumi kwa kununua bidhaa ya hiyo kuwa na uhakika pale wanapopata majanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!