Home Kitaifa WENYE MATATIZO YA MACHO WAENDELEA KUPATIWA HUDUMA ZA KIBINGWA HOSPITALI YA MWALIMU...

WENYE MATATIZO YA MACHO WAENDELEA KUPATIWA HUDUMA ZA KIBINGWA HOSPITALI YA MWALIMU NYERERE

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wenye matatizo ya macho mkoani Mara wameendelea kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa kwenye hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Huduma hizo wanazipata kutoka kwa madaktari bingwa kutoka hospitali ya rufaa ya kanda Bugando kwa kushirikiana na madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo.

Akizungumza hospitali hapo mganga mfawidhi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk.Osmundi Dyegura amesema wananchi wameendelea kupokelewa na kupata huduma zikiwemo za oparesheni.

Amesema madaktari hao wameendelea kuwaona wananchi na kuwafanyia uchunguzi na wanaobainika kufanyiwa oparesheni wanapewa huduma hiyo.

Dk.Dyegura amesema hospitali imekuwa na utaratibu wa kuwaleta madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kila mwezi na safari hii wanao wa magonjwa ya macho na kuwaomba wananchi kuwatumia kupata huduma.

Amesema huduma zimeanza februari 10 na zinaendelea kutolewa hadi ijumaa ya februari 14 na kudai hiyo ni fursa ya wananchi kutotumia gharama kubwa kuwafuata madaktari hao.

” Huu ni utaratibu wa hospitali wa kuwaleta madaktari bingwa kila mwezi ili kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wenye matatizo ya magonjwa mbalimbali.

” Macho ni kiungo muhimu kwenye mwili wa binadamu sasa tunao madsktari bingwa hapa hospitalini wenye matatizo waje na watahudumiwa”,amesema

Baadhi ya wananchi waliofika hospitalini hapo kwaajili ya kupata matibabu wameshukuru utaratibu wa kuendelea kuwaletea madaktari bingwa.

Mmoja wa wenye matatizo ya macho aliyefika hospitalini hapo Wambura Samwel amesema amechunguzwa na kutakiwa kufanyiwa oparesheni na anasubili kufanyiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!