Klabu ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, imefuzu hatua ya robo fainali kwa kishindo baada ya kuichapa timu ya CS Constantine mabao 2-0 katika mchezo wa kundi A uliochezwa kwenye Dimba la Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo wa Simba unaifanya timu hiyo kuongoza kundi A na kushika nafasi ya kwanza ikiwa na alama 13, dhidi ya wapinzani wao wenye alama 12 waliopo nafasi ya pili.
Magoli ya Simba SC yalipatikana katika kipindi cha pili cha mchezo, ambapo goli la kwanza lilifungwa na Kibu Denis Prosper kwa mkwaju mkali uliomshinda mlinda mlango wa CS Constantine. Goli la pili lilifungwa na Leonel Ateba.