Home Biashara WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AELEZA FURSA MBALIMBALI KTK VIWANDA VYA MBOLEA...

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AELEZA FURSA MBALIMBALI KTK VIWANDA VYA MBOLEA NCHINI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Tanzania inahitaji wawekezaji katika eneo la uzalishaji wa mbolea ili kutosheleza mahitahiji nakupunguza asilimia 90 ya uagizaji wa mbole kutoka nje ya nchi .

Waziri Kijaji ameyasema hayo Juni 29,2022 Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kufanya mazungumzo kuhusu kuendela uhusiano wa uwekezaji na Biashara kati ya Tanzania na Ghana na ugeni kutoka nchini Ghana ulioongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Naibu Waziri wa Viwanda.

Ugeni huo umeambatana na Wawekezaji na Wafanyabiashara wakubwa kutoka nchini Ghana ambao wanazalisha bidhaa kwenye maeneo ya Nishati pamoja na Kilimo hasa kwenye mbolea.

Waziri Kijaji amesema wamejadili kuhusu uwekezaji katika eneo la viwanda vya mbolea pamoja na eneo la Nishati ambapo kwa pamoja ni maeneo makubwa ambayo wanafanya nayo kazi.

Aidha amesema kuwa kukiwa na wawekezaji wa kutosha ndani ya taifa kutaweza kuhudumia Afrika kwa ujumla kwa kuwa Tanzania ni lango la kuingilia na kutoka Afrika inaweza kuihudumia Dunia .

“Wawekezaji kama hawa sisi tunawapokea kwa mikono miwili kuhakikisha wanaanza uwekezaji na ninaamini hawana muda mrefu wanakuja kuwekeza ndani ya nchi yetu ili tuweze kujitoshereza kwa mbolea na kuwahudumia wenzetu waafrika kutoka Tanzania”. Amesema 

Naye Naibu Waziri wa Viwanda wa Ghana Mhe. Nana Ama Dokua Asiamah Adjei amesema Ghana inawakaribisha wawekezaji na wafanyanyabiashara kuwekeza nchini humo kupitia Mkataba wa Eneo huru la Biashara (AFCFTA) unaoziunganisha nchi za Afrika na kuziwezesha kufanya biashara baina ya nchi na nchi barani humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!