Home Kitaifa WAZIRI WA AFYA ATOA TAHADHARI YA UGONJWA WA EBOLA NCHINI

WAZIRI WA AFYA ATOA TAHADHARI YA UGONJWA WA EBOLA NCHINI

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu ametoa tahadhari juu ya tishio la ungonjwa wa Ebola nchini Tanzania ambao kwa sasa upo nchini Uganda  baada ya mganga mkuu wa nchi hiyo kutangaza uwepo wa ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salam  Waziri Ummy amesema mikoa ambayo ipo hatarini kupata ugonjwa huo ni kagera,Kigoma na Mwanza kutokana na Mikoa hiyo kuwa karibu na mipaka ya nchi ya Uganda.

Waziri Ummy amesema mpaka sasa nchini Uganda wamegundulika watu 43 walioambukizwa ugonjwa huo na mpaka sasa idadi ya vifo imefikia watu 23 ambapo wameonekana na dalili zote za ugonjwa huo kama kuharisha kutapika homa kali na kutoka damu puani, na washukiwa ambao walikuwa na wagonjwa hao ni 127.

Aidha Waziri Ummy amemalizia kwa kuwahimiza wananchi kutoa taarifa pale watakapo muona mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola ili kuepuka kuenea kwa kasi kwa ugonjwa huo.

Naye mganga mkuu wa serikali Dkt.Aifello Sichalwe amesema kuwa serikali kupitia wizara ya afya inapambana kuhakikisha kuwa inadhibiti ugonjwa huo kwa  kudhibiti  misongamano na kuendelea  kutoa elimu kwa wananchi juu ya dalili na athari za ugonjwa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!