Home Afya WAZIRI UMMY MWALIMU AHITIMISHA ZIARA YAKE SIMIYU, AWAPONGEZA KWA KUBORESHA HUDUMA ZA...

WAZIRI UMMY MWALIMU AHITIMISHA ZIARA YAKE SIMIYU, AWAPONGEZA KWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Na. WAF – Maswa, Simiyu

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ahitimisha ziara yake ya siku Tatu ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo, Halmashauri, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati Kwa lengo la kukagua utoaji wa huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto pamoja na upatikanaji wa Dawa na Vifaatiba.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy ameendelea kusisitiza juu ya utolewaji wa huduma bora kwa kuzingatia Weledi, Maadili ya Taaluma ya Udaktari kwa kufuata miongozo ya utoaji wa huduma pamoja na upatikanaji wa dawa katika.

Waziri Ummy akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa amesema ataweka usawa kwa Madaktari juu ya malipo wanayolipwa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo Daktari anayelipwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na NHIF anatakiwa kulipwa sawa na Daktari aliyopo Wilayani.

Daktari anayelipwa Muhimbili na NHIF ndio tunataka alipwe sawa na Daktari aliyopo Wilayani sababu wote wanasifa sawa ili wanaokaa Wilayani nao waone raha ya kusoma kwa shida, kupambana hadi kuwa Daktari”, amesema Waziri Ummy

Lakini pia, Waziri Ummy amewataka madaktari hao kutoa huduma nzuri kwa wananchi kwakuwa Serikali inawapambania kupata haki zao na wao wapambane kutoa huduma bora.

Katika ziara yake Waziri Ummy ametembelea katika Chuo cha Maafisa Tabibu Maswa ambapo amesema kuwa Serikali inampango wa kuweka Skills Lab pamoja na ukarabati wa miundombinu katika chuo hicho.

Tutahakikisha tunaweka Skill Lab katika chuo hiki pamoja na ukarabati wa miundombinu ikiwemo majengo ili kuwafanya wanafunzi wetu wasome katika mazingira mazuri na rafiki kwao”, amesema Waziri Ummy

Hata hivyo, Waziri Ummy ameupongeza sana Mkoa wa Simiyu kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa, kupunguza vifo vya Kina-mama na Watoto chini ya miaka Mitano pamoja na upatikanaji wa dawa.

Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haya yote anayafanya kwakuwa anawajali wananchi wake, hakuna kitu muhimu katika maisha kama Afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda amesema kwa Mwaka huu 2023 kimetokea kifo Kimoja cha mama mjamzito katika Wilaya ya Maswa.

Baada ya jitihada za kupunguza vifo vya Kina-mama Lakini pia, tumeweza kupunguza vifo vya watoto kutoka vifo 67 hadi vifo 18 kwa Mwaka huu, haya ni mapinduzi makubwa sana katika Wilaya ya Maswa, lakini Kimkoa kwa Mwaka huu tumepoteza Kina-mama 12 tu na tunaendelea kujitahidi tuendelee kupunguza vifo na kupeleka huduma kwa wananchi kwa wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!