Home Afya WAZIRI UMMY AWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU UGONJWA WA MARBUG ASISITIZA JUHUDI ZA...

WAZIRI UMMY AWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU UGONJWA WA MARBUG ASISITIZA JUHUDI ZA KUUDHIBITI ZINAENDELEA KWA KASI

Na Theophilida Felician, Kagera

Waziri wa afya Ummy Mwalimu ameuhakikishia umma kuwa jitihada za Serikali chini ya wizara ya Afya katika kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Marbug uliolipuka hivi karibuni Mkaoni Kagera zinaendelea vyema kwani tangu kutokee visa vya watu wa 8 waliougua ugonjwa huo tangu tarehe 15 mwezi huu hadi sasa hakujaongezeka tena visa vya watu wengine.

Akitoa taarifa ya mwenendo wa ugonjwa huo kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi ya Mkoa Kagera Manispaa ya Bukoba amezitaja njia mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuendelea kuudhibiti ipasavyo ikiwemo ya kuweka vipimo vya homa katika maeneo ya viwanja vya Ndege, vituo vya Mabasi, Bandari, kutuma timu ya watalaamu wa fya kwenda visiwa vya Goziba alikotokea mgonjwa wa kwanza katika kufuatilia kama kuna watu wenye dalili za ugonjwa huu hiyo ikiwa ni sambamba na kueneza elimu kwa wananchi namna ya kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi.

Tumepata meli iko kule itapita kwenye visiwa itapita nyumba kwa nyumba, vitongoji kwa vitongoji, itapita vijiji kwa vijiji, mitaa kwa mitaa timu zetu tumeziimalisha sawa sawa kama mtaona watu wanaoingia na kutoka Kagera wameanza kupimwa nashukuru jana nimepata taarifa ya waziri mwenzangu wa afya wa Uganda Dr Jenni akiniarifu kuwa alivyofika mpakani mwa Mtukula amepimwa hii ni hatua nzuri nauhakikishia umma na jumuia ya kimataifa kwamba Serikali inachukuwa hatua zote za kuhakikisha ugonjwa huu tunaumaliza ndani ya muda mfupi” ameeleza Waziri Ummy mbele ya waandishi wa habari.

Amesema kuwa mwelekeo wa Serikali katika kuudhibiti ugonjwa wa Marbug na magonjwa mengine ya kuambukiza na yamlipuko ni kuishirikisha jamii hususani kupitia wahudumu wa afya ngazi ya jamii, viongozi wa dini na waganga wa tiba ya asili pamoja na kuwaajili kwa muda wa miezi mitatu wahudumu wa afya (1322) watakaowekwa katika Vijiji, vitongoji na mitaa Mkoani Kagera.

Ameeleza kuwa wamechukua hatua ya kuwaajili watu hao ili waweze kusaidia kuongeza nguvu ya kuifikisha elimu zaidi kwa wananchi jambo ambalo litawezesha kuutokomeza kwa haraka ugonjwa huo.

Hata hivyo ameongeza kwamba kati ya watu 8 waliokumbwa na ugonjwa huo watu watano walipoteza maisha na wengine wa 3 wanaendelea na matibabu katika vituo vya kutolea tiba na watu 205 waliotangamana na wagonjwa hao wametengwa wakiendelea kufuatiliwa kama wanaweza kuwa na viashiria vya virusi vya ogonjwa wa Marbug japo hawaumwi na watu hao ni wanafamilia waliouguza wagonjwa pamoja na watumishi wa afya waliowahudumia wagonjwa wenye ugonjwa huo.

Waziri Ummy akiambatana na Dr Zabroni Yoti Mwakilishi mkazi wa shirika la afya Dunia (WHO) pamoja naye Bi Shaini Bahuguna mwakilishi wa shirika la watoto Duniani (UNICEF) kuelekea kata za Maruku na Kanyangereko Halmashauri ya Bukoba ulikotokea ugonjwa huo amewatoa hofu wananchi akiwasihi kuendelea kufanya shughuli za maendeleo huku wakichukua hatua madhubuti za kujikinga na maambukizi.

“Nilivyofika hapa nimefurahi wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida hili nataka kulisisitiza shughuli za kiuchumi ziendelee hakuna haja ya kuwa na hofu hakuna haja ya kuwa na wasi wasi isipokuwa wananchi ninawataka na kuwahimiza wazingatie maelekezo ya watalaamu juu ya hatua zakujikinga na ugonjwa huu tuepuke kushika mizoga kama kuna mgonjwa ametokea tupige simu, kunawa mikono kwa maji na sabuni au kutumia vitakasa mikono” Waziri Ummy akihitimisha hotuba yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!