Home Afya WAZIRI UMMY AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

WAZIRI UMMY AWATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI

Na Boniface Gideon -TANGA

Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga amewataka Wanawake na Vijana kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazowazunguka ili kujikwamua kiuchumi,
Waziri Ummy pia amewapiga jeki Wanawake wa Jiji la Tanga waliopo kwenye jukwaa la Wanawake Wilaya ya Tanga kwakuchangia Sh. 5,000,000.

Akizungumza leo, wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Tanga ambapo pia walifanya Uchaguzi wa viongozi wapya baada ya waliokuwepo kumaliza muda wao wa Utumishi wa miaka mitatu, Waziri Ummy amesema huu ni wakati wa Wanawake kuamka na kuchangamkia fursa za kiuchumi ikiwemo Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa Makundi ya Wanawake, Wenye Ulemavu na Vijana.

“Serikali imerejesha Mikopo ya Halmashauri na kuanzia Julai itaanza kutolewa, hivyo niwaombe Wanawake wenzangu tuchangamkie Mikopo hii ili tukakuze Biashara zetu na tuondoe utegemezi kwa akinababa” amesisitiza Ummy

Amewataka watakaochukua Mikopo hiyo kuacha tabia ya kufanya anasa kwa kutumia fedha za Mikopo hiyo.

“jamani tuelewane hii ni Mikopo na mkopo sharti lake ni lazima urejeshwe, msije mkachukua Mikopo alafu mkaenda kufanyia sherehe, lakini pia huko mtaani Kuna fursa nyingi sana, kwa hiyo zichangamkieni na muwe wabunifu katika kazi zenu ili ziingie kwenye soko la ndani na Kimataifa” Amesisitiza Ummy

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmshauri ya Jiji la Tanga Dkt. Frederick Sagamiko aliwataka Wanachama wa jukwaa hilo kuwa mfano kwa Wanawake wengine katika uwekezaji.

“Halmshauri imeweka mikakati dhabiti ya Mikopo, tunaamini itawanufaisha Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu, hivyo niwaombe mkawe mfano kwa wengine, fanyeni ubunifu wa miradi ya Kiuchumi ambayo itawanufaisha katika vikundi na mtu mmoja mmoja ili mjikwamue kiuchumi” Amesisitiza Dkt. Sagamiko

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!