Home Kitaifa WAZIRI UMMY AMUAGA BALOZI WA IRELAND, UK, CANADA

WAZIRI UMMY AMUAGA BALOZI WA IRELAND, UK, CANADA

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu hapo jana Julai 30, 2024 amemshukuru na kumuaga Balozi wa Ireland Mhe. Mary O’Neil, Balozi wa UK Mhe. David Concar pamoja na Balozi wa Canada Mhe. Kyle Nunas baada ya kumaliza muda wao wa utumishi hapa nchini.  

Wakati wa kikao hicho kilichofanyika kwa nyakati tofauti katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dar Es Salaam, Waziri Ummy amesema Nchi hizo zinashirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za Afya ikiwemo kuchangia katika Mfuko wa Afya wa Pamoja ambao lengo kubwa ni kuboresha huduma za Afya ya Msingi.

“Maeneo mengine tunayoshirikiana nao ni katika huduma za Afya ya uzazi, mama na mtoto, Afya ya vijana ikiwa ni pamoja na kupunguza mimba za umri mdogo, uzazi wa mpango, kuimarisha huduma za HIV, TB, Maleria pamoja na Tafiti za Afya.” Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amewaomba Mabalozi hao kuendeleza ushirikiano hata kipindi ambacho wanaendelea na majukumu nje ya nchi ya Tanzania hususan katika eneo la utengemao na shufaa kwa watoto kwa eneo la Tiba Kazi, Tiba za Lugha (Speech therapy), Tiba Viungo, rasilimali watu, kugharamia wasio na uwezo pamoja na eneo la magonjwa Yasiyoambukiza.

Kwa upande wa Mabalozi hao wote kwa pamoja wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Wizara ya Afya kwa kuonesha ushirikiano mkubwa kwa Balozi hizo ambapo wameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kwa kwenda kuwaeleza wenzao wajao ili na wao waendelee kutoa ushirikiano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!