Home Kitaifa WAZIRI ULEGA ACHANGIA UJENZI WA UKUMBI WA CCM MKOA WA PWANI BOKSI...

WAZIRI ULEGA ACHANGIA UJENZI WA UKUMBI WA CCM MKOA WA PWANI BOKSI 200 ZA MALUMALU

Na Scolastica Msewa, Kibaha.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga amemaliza ahadi yake aliyoitoa Kwa Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kukabidhi boksi 150 za Malumalu alizoahidi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya CCM Mkoa wa Pwani.

Akizungumza Katika zoezi la kukabidhi Malumalu hizo katika ofisi za CCM mkoa Kibaha mkoani Pwani Waziri Ulega amesema dhamana aliyopewa na Mhe. Daktari Samia Suluhu ni heshima kubwa kwa Mkoa wa Pwani hivyo hana budi kujitoa kikamilifu kukichangia Chama na kusisitiza kuwa ndicho kilichomlea tangia akiwa kiongozi wa Vijana wa CCM mkoani humo.

“Ndugu zangu Wana CCM na Wana Pwani leo nafasi niliyonayo ni kwa sababu nimelelewa na CCM na kuonyesha nidhamu kubwa hivyo nakipenda sana Chama changu” amesema Waziri Ulega.

Alisema kuwa Bado yeye na Familia yake wataendelea kuhakikisha Ujenzi huo unakamilika hatua Kwa hatua hadi ofisi hizo zitakapokamilika ambapo awali alichangia boksi 50 na kufanya Jumla ya boksi 200.

Aidha Ulega aliwaasa wale wote wanaoahidi kujitahidi kutimiza ahadi zao ili Ofisi hiyo mpya ya CCM iweze kumalizika na kuanza kutumika mapema iwezekanavyo.

Aidha kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Bernard Ghaty amemshukuru Ulega kwa kuonyesha moyo wa kukipenda Chama kwa vitendo na kumtakia utendaji uliotukuka katika majukumu yake.

Pamoja na mambo mengine Katibu Ghaty amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuonyesha mfano katika kuleta maendeleo nchini.

Kwa upande wake Katibu wa Uchumi Kamati ya Ujenzi wa Ukumbi na Ofisi ya Chama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri Ally amempongeza Waziri Ulega Kwa hatua hiyo na kuwaomba wadau wengine kumaliza ahadi walizozitoa Ili kufanikisha kumalizika Kwa Ujenzi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!