Home Kitaifa Waziri Simbachwene ahimiza mapambano dhidi ya udhalilishaji wanawake na watoto

Waziri Simbachwene ahimiza mapambano dhidi ya udhalilishaji wanawake na watoto

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ametoa wito kwa Walezi na jamii kwa ujumla kupiga vita dhidi ya udhalilishaji kwa Wanawake na Watoto mambo ambayo yanapoteza heshima na haiba kwa nchi yetu.

“tushirikiane katika kutokomeza udhalilishaji kupinga, kuwafichua na kuwafikisha katika vyombo vya Sheria wale wote wanaofanya unyama huu kwa wanawake na Watoto, lakini pia hatunabudi kurejesha utamaduni wetu wa malezi ya pamoja ili kulidhibiti janga hili kwa jamii na Taifa kwa ujumla.”

wito huo ameutoa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa kituo cha afya Shehia ya Uzi Mkoa wa Kusini Unguja katika sherehe ya kuadhimisha miaka 59 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar siku ya tarehe: 06/01/2023.

Katika shughuli yetu kuu ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wetu huu, ambayo tayari tumeshaifanya kwa ukamilifu wake, hivyo iliyobaki kwetu ni kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa hatua zilizobakia ili kukidhi malengo tuliyoyakusudia.

tunaendelea kushuhudia mapinduzi makubwa ya kiuchumi yanayoendelea kufanyika nchi nzima na hii inathibitisha kauli ya mwaka huu isemayo “Mapinduzi yetu ndio Amani yetu tuyalinde kwa Maendeleo yetu”.

Aidha serikali zetu zote mbili ya SMT na SMZ zimeendelea kusogeza huduma mbalimbali kwa wananchi wake na tunashuhudia ujenzi wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo huu wa ujenzi wa Kituo cha Afya katika Shehia zetu za Uzi na Ng’ambwa. Mradi ambao unafadhiliwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF ambao ni miongoni mwa matunda ya Mapinduzi yetu yaliyofanyika Januari 12 mwaka 1964.

“ujenzi huu wa Kituo cha Afya umekuja baada ya kuona upo uhitaji mkubwa wa jengo hili kwa wanajamii wa Shehia zetu za Uzi na Ng’ambwa, hali ambayo itarahisisha upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wananchi hususani mama na watoto,”alisema Waziri.

Waziri amesisitiza ushirikiano wa hali na mali katika ufuatiliaji, usimamizi na utekelezaji wa mradi ili uweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu. Pia, amewaomba viongozi wa Mkoa, Wilaya, Baraza la Mji Kati na Shehia zote kuwa karibu katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa jamii na Taifa kwa ujumla na kuendelea kutoa msaada pale unapohitajika ili kufanikisha ukamilishaji wa mradi kwa wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!