Home Kitaifa WAZIRI SIMBACHAWENE : KUKOPA SI AIBU, NI AFYA KIUCHUMI

WAZIRI SIMBACHAWENE : KUKOPA SI AIBU, NI AFYA KIUCHUMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema mikopo ni moja ya vyanzo vya mapato ya serikali kote duniani, hivyo Tanzania kukopa siyo aibu wala kujidhalilisha, bali ni sifa njema kwa kuwa inakopesheka.

Simbachawene ametoa kauli wakati akizungumza kwenye harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kubadilisha paa la Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu,Yuda Tadei Mang’ola Chini, Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, ambalo limekuwa likivuja wakati wa mvua na hivyo kusababisha wakristo kushindwa kukaa ndani.

Amesema vyanzo vya mapato vya Kanisa ni pamoja na sadaka ya kila jumapili, zaka, misaada mbalimbali pamoja na harambee huku akitaja vyanzo vya mapato vya Serikali kuwa ni kodi, tozo, misaada na mkopo, na kusema kukopa ni moja ya chanzo cha mapato ya serikali na serikali zote duniani zinakopa.

Aidha amesema kama ingetokea Tanzania haiwezi kukopesheka hiyo ndo ingekuwa aibu lakini kwa kuwa inakopsheka hiyo ni heshima kubwa kwa watanzania kwa kuwa inakopa ili kutekeleza miradi ya maendeleo na kama isipofanya hivyo itapelekea nchi kupata madhara makubwa ambayo yasingetokea kama ingekopa.

Amesema Nchi zote duniani ikiwemo Marekani na China zinakopa na zinadaiwa na kwamba kodi inayokusanywa nchini haina uwezo wa kutekeleza miradi hiyo na kama kodi hiyo itaweza kutumika inaweza kuchukua zaidi ya miaka 40 ili kukamilisha miradi hiyo.

Vyanzo vya mapato vya Kanisa ni sadaka ya kila jumapili, zaka, misaada mbalimbali pamoja na harambee ambapo harambee ni hatua ya mwisho ya utafutaji wa fedha kwa Taasisi za dini, lakini vyanzo vya mapato vya Serikali ni kodi, tozo, misaada na mkopo, hivyo kukopa ni moja ya chanzo cha mapato ya serikali na serikali zote duniani zinakopa”amesema Simbachawene na kuongeza kuwa

Kukopa ni chanzo cha mapato hivyo isionekane Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inapokwenda kutafuta mkopo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo ndo inakopa sana”.

Amesema kutokana na mahitaji makubwa ya nchi suala la kukopa haliepukiki akitolea mfano uendelezaji wa Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere ambalo gharama yake ni zaidi ya trioni 6 huku bajeti ya Serikali ya mwaka mzima ikiwa ni tirioni 43 huku zaidi ya asilimia 7O ya fedha hizo zikitumika kwa ajili ya uendeshaji wa nchi na asilimia 30 ndizo hupelekwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo

Hivi tungetaka kujenga reli ya SGR kwa kodi yetu tungejenga kwa miaka mingapi?amehoji Simbachawene na kusema ikijengwa kwa miaka 100 itakuwa na tija kweli na tukiamua tutaweza kujenga kwa miaka 50 au 60 ambapo hapo tutaacha kulipana mishahara, kusomesha watoto pamoja na kutibu wagonjwa

Amesema “Mbali na utekelezaji wa miradi hiyo ya kimkakati, Serikali chini Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea na ujenzi wa madarasa ambayo ili kumaliza upungufu wa madarasa uliopo sasa kama zisipokopwa changamoto hiyo itatuliwa ndani ya kipindi cha zaidi ya miaka 25 ijayo huku idadi ya watu ikizidi kuongezeka“.

“Unataka Rais Samia akae tu asiende kukopa” amehoji Simbachawene na kususitiza kuwa,

Kukopa ni chanzo cha mapato na kukopa sio kujidhalilisha, Tanzania ina sifa hiyo ya kukopa. Nchi inayoweza kukopesheka ni nchi yenye heshima kama ilivyo Tanzania kwani mashirika makubwa ya fedha duniani ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la fedha Duniani ( IMF) zimeweka vigezo za vya kuweza kukopesheka na Tanzania inakopesheka kwa sababu ina vigezo”.

Hata hivyo Mhe.Simbachawene amesema kwa mujibu wa kanuni za fedha duniani zinaipa Tanzania wigo wa ukomo wa kukopa na kama nchi bado ina sifa ya kukopa kwa sababu bado haijafikia kikomo hicho.

Amesema “Hivi reli ikishajengwa inarudia tena kujengwa , umeme ukianza kuzalishwa tunarudia tena, viwanja vya ndege, madaraja, madarasa na vituo vya afya vinavyojengwa nchi nzima havirudiwi tena kujengwa na hivi ndo vinajenga uchumi kisha tunasonga mbele” amesema Simbachawene

Fedha hizi zinazokopwa ni muhimu kwa maendeleo ya nchi huku akitolea mfano Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Dodoma ndani ya kipindi cha miaka mitatu chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan haikuwahi kupata fedha nyingi za maendeleo ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita“.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!