Home Kitaifa WAZIRI SIMBACHAWENE AKAGUA MAANDALIZI YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA:

WAZIRI SIMBACHAWENE AKAGUA MAANDALIZI YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA:

Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene pamoja na Kamati Tendaji ya maandalizi ya Maadhimisho Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa wametembelea na kukagua maandalizi ya kuelea Siku hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Batholomeo Jungu alipotembelea kukagua maandalizi ya kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa, yatakayofanyika Kitaifa Jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa Jijini Dodoma katika la Uwanja wa Mnara wa Mashujaa tarehe 25 Julai, 2022 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Vikosi mbalimbali vya Ulinzi na Usalama vikiwa katika mazoezi wakati wa maandalizi ya kuelekea Madhimisho ya siku ya Mashujaa Jijini Dodoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!