Home Kitaifa PROF MKENDA: MAKTABA TATU NCHI NZIMA HAZIKIDHI MAHITAJI KWA WASOMAJI

PROF MKENDA: MAKTABA TATU NCHI NZIMA HAZIKIDHI MAHITAJI KWA WASOMAJI

Na Magrethy Katengu

Bodi ya Maktaba imeshauriwa kushirikiana na halmashauri, mashule na Tamisemi kuanzisha Maktaba za jumuia kwani 3 zilizopo nchi nzima hadhikidhi mahitaji ya wasomaji vitabu na kupelekea hali halisi ya vizazi kusoma nyaraka kama ilivyo miaka ya nyuma kupoteza dira.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adlof Mkenda wakati alipotembelea Maktaba kuu ya Taifa ambapo amesema Maktaba ina umuhimu mkubwa sana kwa jamii kwani kupitia usomaji wa vitabu na nyaraka mbalimbali husaidia kubadilisha fikra za mtu na kuwa mtazamo mzuri kufikia mafanikio .

“Kuna changamoto kubwa uandishi na usomaji wa vitabu kutoka na wanaochapa vitabu kukosa soko hivyo waandishi wanapata shida na wengine wanaingia mfukoni kugharamia na wengine kuacha kabisa hivyo Mimi na katibu wangu tumejaribu kuipunguza changamoto hiii kwa kuanzisha uandishi wa tuzo ya Mwalimu Nyerere na mshindi kitabu chake kinanunuliwa na kuwekwa maktaba watu wasome” amesema Prof Mkenda

“Miaka ya nyuma wakati Mimi nasoma kulikuwa hakuna hata jengo moja la maktaba kijijini kwetu Mpshi ila walikuwa wanatumia majengo ikiwemo ya kanisa katika na sehemu mbalimbali ambapo wafunzi tukitoka shuleni tunawahi kuazima vitabu na kujisomea historia za watu marufu, pamoja na masomo yetu desturi hii ilikuwa inatujengea kubadilisha fikra zetu na kupenda zaidi usomaji wa vitabu lakini kwa sasa hakuna majengo hayo vijijini je kizazi chetu kinakwenda wapi ikiwa hali ya usomaji imepungua na wachapishaji hawachapishi kutokana na kukosa soko la kuuza machapisho yao” amesema Waziri

Sambamba na hayo amesema Elimu yetu haitabaki kwa kutegemea vitabu tunavyoandika wenyewe hivyo katika maktaba inakiwa bodi hii ihakikishe kunakuwa na vitabu vya aina tofauti na vitabu vya Watanzania wenzetu ambao wameviandika kwa lugha ya kingereza vifasiliwe kwa kiswahili, na lugha nyingine hadi na hivyo lazima bodi iangalie je miaka hii vijana waliopo vijijini wanapata fursa ya kusoma vitabu .

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makataba Dkt Mboni Ruzegea amesema wamekuwa na chuo cha na Ukutubi na Uhifadhi nyaraka kilichopo Bagamoyo ambapo kinasadia kuwapika watumishi bora ili kutekeleza dira mpya ya Tanzania kuwa jamii iliyoelimika ili kumudu changamoto za mabadiliko hivyo kupiti usomaji wa vitabu vilivyopo itasaidia.

“Maktaba ni chombo muhimu na Moyo katika Taifa hususani kukusanya na kuhifadhi nyaraka kuwapatia walengwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo kwani Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema vitabu njia nzuri katika kujiendeleza kujitegemea kwani tunaweza kujifunza mbinu mpaya, kuongeza wigo mpya wa uwelewa kupitia historia za watu wengine waliofanikiwa “ amesema Mkurugenzi

Naye Mkurugenzi wa taasisi Mipango na Uwekezaji Maktaba Gerald Nzalila amesema katika kipindi cha mwaka 2021/2022 serikali ilitengea bodi ya Maktaba kiasi cha fedha cha bilio 1 na Milioni 417 na laki 650 zikiwa ni fedha kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi na shughuli za huduma zote .

Aidha Wito umetolewa kwa watu wote kuwa wasomaji wa vitabu kwani kuna maarifa mengi ambapo itasaidia kujua historia za watu waliofanikiwa changamoto walizokumbana nazo lakini walipambana na wakafanikiwa na historia zao wakaziandika ili ziwasaidia vizazi vijazo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!