Home Kitaifa WAZIRI NAPE AFTURISHA JIMBONI

WAZIRI NAPE AFTURISHA JIMBONI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye amefuturisha wananchi wa Jimbo la Mtama ikiwa ni sehemu ya kila
mwaka kufanya jambo hilo katika kipindi cha Mfungo wa Ramadhan.

Pia Waziri Nape aliungana na Wananchi wa Mtama kuliombea dua Taifa letu la Tanzania pamoja na kumuombea Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan awe na afya njema na aweze kuendelea kuliongoza vema Taifa.

Katika hatua nyingine Waziri Nape ametumia Hafla hiyo kuwakumbusha wakazi hao wa Mtama kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru utakaopokelewa Jimboni hapo kesho Tarehe 11 Aprili, 2023.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!