Home Kitaifa WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN MALECELA NA MBUNGE WA JIMBO LA SAME MASHARIKI...

WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN MALECELA NA MBUNGE WA JIMBO LA SAME MASHARIKI WAFANYA ZIARA KIJIJI CHA MAKOKANE KATA YA KALEMAWE ATOA MILIONI 1.5 KUUNGA MKONO JITIHADA ZA WANANCHI HAO KATIKA KUJILETEA MAENDELEO.

Na Dickson Mnzava, Same.

Mhe Makamu mwenyekiti wa ccm Tanzania bara na Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Jonh Malecela mguu kwa mguu akiwa na mkewe mhe Anne kilango malecela(MB).
Amekitembelea kijiji cha makokane Kilichopo kata ya Kalemawe ndani ya jimbo la same mashariki kwa ajili ya kuona juhudi za wananchi wa kijiji hicho katika kujiletea Maendeleo bila kusubiri fedha za serikali.

Hakika juhudi hizo zimemkosha sana Mzee Malecela na kuwiwa kuwachangia fedha kiasi cha Ts1,500,000/= milioni moja na laki tano fedha ambazo zitasaidia kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi wa kijiji hicho.

Aidha Mzee Malecela aliwasihi waendelee kuwa wamoja na mshikamano kwani zahanati hiyo inakwenda kuwa mkombozi wao na kwa kizazi kijacho kwani itaenda kuondoa adha ya upatikanaji wa huduma ya afya kwa wananchi wa kijiji hicho.

“Pia niwaombe wananchi kuiunga mkono serikali ya Chama cha mapiduzi inayoongozwa na Jemedari Daktari Samia Suluhu Hassani Rais wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mimi pamoja na mbunge wenu tuko bega kwa bega na ninyi kuhakikisha tunawaunga mkono juhudi zenu zote za maendeleo na hakika hakuna kitakacho shindikana “
“Amesema Mzee Malecela”.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!