Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Leo Novemba 23, 2023, ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe, iliyopo katika kijiji cha Hassamba Kata ya Vwawa, Wilaya ya Mbozi.
Mradi huo hadi sasa umetumia bilioni 13 na hadi kukamilika unatarajia kutumia Bilioni 16.7. Baadhi ya majengo ya Hospitali hiyo yamekamilika na mengine yako katika hatua ya ukamilishaji
Hospitali hiyo imeanza kutoa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe na Nchi za jirani ambapo hadi sasa wagonjwa 19,265 wamehudumiwa.