Home Kitaifa WAZIRI MKENDA AZINDUA MRADI WA HEET UTAKAONUFAISHA VYUO 14

WAZIRI MKENDA AZINDUA MRADI WA HEET UTAKAONUFAISHA VYUO 14

Na Magrethy Katengu

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali itahakikisha inawasomesha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu nje ya nchi Ili kusaidia kutoa elimu ujuzi yenye kiwango bora kuendana na soko la ajira kimataifa.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizindua Mradi wa HEET wa miaka mitano uliolenga kuboresha elimu na kunufaisha vyuo 14, uzinduzi umefanyika leo Septemba 13,2022 Jijini Dar es Salaam

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa HEET wa miaka mitano 2021hadi 2026 uliolenga kuboresha elimu na kunufaisha vyuo 14 ambapo amesema kupitia mradio pia unakwenda kusaidia Wahadhiri kwenda kusoma katika nchi mbalimbali ikiwemo Denmark,Ufaransa,Ubelgiji, Ili kusaidia kuongeza ubora wa Elimu na lazima ianzie juu ndipo ishuke sekondari hadi shule za msingi kwani dunia Sasa hivi imebadikika kinachohitajika ni ujuzi zaidi.

“Duniani kote wanazungumzia suala la elimu hii inatokana na changamoto ya kuwa na wahitimu wengi lakini wanaoshindwa kujiajiri kutokana na kutokuwa na ujuzi ukitazama vyeti wanavyo lakini digree za kutosha lakini mwanafunzi inashindikana kuajiajiri hivyo Wahadhiri waliopata fursa kwenda kusoma njee wakihitimu wanaokuja kubadilisha mtazamo”amesema Waziri

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa HEET wa miaka mitano uliolenga kuboresha elimu na kunufaisha vyuo 14 uliyofanyika Dar es salaam

Sanjari na hayo Waziri amesema Mradi huo ni mkubwa na ni wa kipekee ambao umekuja kutoa hamasa na kusukuma Tanzania katika suala zima la elimu ikiwa ni pamoja na uboreshajiwa miundombinu ya vyuo ikiwemo mitaala.

Naye Katibu mkuu wa Wizara ya elimu Sayansi na Teknolojia Dk Francis Michael amewataka wasimamizi wa mradi kuhakikisha fedha zikizotolewa za mradi zinatumika katika mlengo uliokusudiwa kwani ikibainika kuna ujanja ujanja watakaohusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa HEET wa miaka mitano uliolenga kuboresha elimu na kunufaisha vyuo 14 uliyofanyika leo Septemba 13,2022 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Michael amebainisha kuwa fedha zikizotolewa jumla ya Milion 425 sawa na Bilioni 972 zimetolewa na Benki ya dunia ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu Kwa lengo la kuboresha elimu ya juu.

” Bado Vyuo vikuu havijafikia kiwango kilichowekwa kwa wahitimu wa elimu ya juu kwani mpaka sasa ni asilimia 3.5 ambapo lengo ni kufikia asilimia 12.
naitaka kamati ya wasimamizi wa mradi huu kutosita kutoa taarifa ya changamoto yeyote itakayowakabili ili kuenda sambamba na kasi ya utekelezaji “amesema Mkenda

Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Bi.Preeti Arora akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa HEET wa miaka mitano uliolenga kuboresha elimu na kunufaisha vyuo 14 uliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Naye Mwakilishi kutoka benki ya Dunia Preeti Arora ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na mtazamo chanya wa kuboresha elimu Ili kuendana na mahitaji ya Soko la ajira la kimataifa hivyo watahakikisha wanashirikiana nao began kwa bega pale watakapohitajika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!