Home Kitaifa Waziri Mhagama ashiriki Msiba wa aliyekuwa Diwani Mbinga Mhalule

Waziri Mhagama ashiriki Msiba wa aliyekuwa Diwani Mbinga Mhalule

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika Sera, Bunge na Uratibu (Mb.) Peramiho Mhe. Jenista Mhagama ameshiriki katika Mazishi ya Marehemu Nasri Nyoni aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mbinga Mhalule Iliyopo Halmashauri ya wilaya ya songea vijijini Mkoani Ruvuma.

Katika ibada hiyo mazishi iliyofanyika katika Kijiji cha Matomondo Waziri Mhagama ametoa pole kwa Mwenyekiti wa Halmashauri wilaya ya Songea vijijini na wafiwa wote.

“Mimi kama Mbunge na Diwani nimepoteza Mwenzangu Marehemu, Nasri alikuwa rafiki yangu kikazi, na tumeshirikiana sana kuleta maendeleo katika kata hii na nyinyi wananchi ni mashahidi tukisimamiwa na ilani ya Chama Cha Mapinduzi,”alibainisha

Naomba niwahakikishie Wanambinga Mhalule mnao ushirikiano wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu, wote wako pamoja wako na nyie.

Aliendelea kusema kuwa serikali itaendelea kuhakikisha Mbinga Mhalule inaendelea kusonga mbele kama alivyokuwa anasimamia aliyekuwa Diwani wa mbinga Mhalule, ili kuendelea kumuenzi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Ndg. Odo Mwisho amesema jambo kubwa ni kuendelea kufarijiana na kuendelea kumuombea Mwenzetu aliyetutangulia.

“Amefanya mambo mengi wa kushirikiana na wananchi na sisi tumeona, tunamatarajio makubwa sana kwamba katika haya maisha ambayo ameyaanza ataenda kupata utukufu” alifafanua Mwenyekiti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!