Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa amekabidhiwa rasmi kadi ya uwanachama wa Klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Gofu na kuanza Mazoezi ya Mchezo huo kwa mara ya kwanza.
Akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi katika klabu hiyo Waziri Mchengerwa amesema, amevutiwa na mchezo huo ikiwa ni sehemu moja ya mazoezi na ajira hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuucheza Mchezo huo pamoja na Michezo mengine.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema,Mh Waziri ameonesha umahiri mkubwa wa kuucheza Mchezo wa Gofu huku akiwaomba viongozi mbalimbali na Watanzania kujifunza Mchezo huo.
Naye Mkufunzi wa Klabu hiyo Geoffrey Levirian amesema,Ingawa ni mara ya kwanza kwa Waziri Mchengerwa kucheza Mchezo wa Gofu na ameshangwazwa na kiwango alichokionesha Wakati akifanya mazoezi.
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa pia amesaini fomu ya kujiunga na Klabu hiyo na kukabidhiwa kitabu Cha sheria za Mchezo wa Gofu na Nahodha wa klabu ya Lugalo Meja Japhet Masai.