Waziri wa Sanaa , Utamaduni na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akikabidhi bendera ya Tanzania kwa baadhi ya washindi wa promosheni ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense ambao wanaenda kushuhudia kombe la Dunia nchini QATAR mapema leo hii katika Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar Es Salaam.
Balozi wa Kampeni ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense , Aishi Manula katika picha ya pamoja na Baadhi ya Washindi , muda mchache kabla ya kuanza safari.
Msafara wa magari yaliyowabeba baadhi ya Washindi wa Promosheni ya WAKISHUA TWENZETU QATAR NA Hisense ulivyowasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar Es Salaam tayari kwa safari.
Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Sanaa , Utamaduni na Michezo Mhe. Mohammed Mchengerwa ameipongeza kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika michezo , hasa kupitia kampeni ya WAKISHUA TWENZETU QATAR NA Hisense , ambayo kampuni hiyo imeiendesha na kupata washindi takribani 50 kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao wamepata nafasi ya kwenda kushuhudia mechi za kombe la dunia nchini Qatar huku wakilipiwa kila kitu na kampuni ya Tigo .
Akizungumza wakati wa kuwaaga washindi 10 wa mwanzo ambao wameanza safari ya kwenda Qatar Leo , Novemba 29 , 2022 Waziri Mchengerwa amesema kuwa
” Kiukweli niipongeze sana kampuni ya Tigo kwa kuamua kurudisha kwa watanzania kupitia kampeni mbalimbali wanazozifanya niwapongeze sana , hapa leo mbele yangu Washindi 10 kati ya 50 wanaanza safari leo ya kwenda Qatar , hii ni furaha kubwa kwao binafsi lakini pia kwa nchi kiujumla maana hawa wanaenda kujifunza na watakuja na mawazo mapya ya nini na sisi kama Tanzania tufanye kujiboresha zaidi ili nasisi tuweze kufikia lengo la kushiriki katika mashindano haya ya Kidunia , na sisi kama Wizara Milango yetu iko wazi , tupo tayari kupokea ushauri watakaotuletea kwa maana Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan anafanya Jitihada kubwa za kuboresha sekta ya Michezo ”
Aidha nawasihi mkawe mabalozi wazuri wa Tanzania huko muendako , tunategemea kuona matunda ya nyinyi kwenda huko pale mtakaporudi , Asanteni sana Tigo kwa kuliwezesha hili”. Alimalizia
Aidha Naye , Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha amemshukuru Waziri Mchengerwa kwa ushirikiano na kuongezea kuwa
” Washindi hawa 10 ni kati ya wale washindi 50 wa Kampeni nzima , kwahiyo watakua wakiondoka kwa awamu ambapo zitakua jumla ya awamu tano “
Lakini pia Mhe. Waziri si ivyo tu maana katika kampuni hii ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense , Licha ya kuwapata washindi hawa 50 wa kwenda kutazama kombe la dunia , pia kuna wengine wengi tu ambao wamejishindia na wanaendelea kujishindia vifaa vya ndani vya Hisense ambavyo ni TV inchi 50 , Subwoofer , Microwave na Friji “
Aidha nichukue nafasi hii kuipongeza kampuni ya Hisense kwa kushirikiana nasi katika kulifanikisha hili , Kampeni bado inaendelea kwahiyo endeleeni kufanya miamala mingi iwezekanavyo kupitia TIGO PESA APP au piga *150*01# ili kuibuka mshindi wa zawadi za pesa taslimu ( milioni 1 kila wiki , Milioni 5 kwa mwezi wa Disemba , na zawadi kuu za pesa taslimu Milioni 10 na Milioni 20 ) , Vifaa vya Ndani vya Hisense na gari jipya kabisa aina ya Toyota Rush “. Alimalizia Bi. Pesha.