Home Kitaifa WAZIRI MBARAWA AFUNGUA BARABARA YA JUU KURAHISISHA SHUGHULI ZA UJENZI

WAZIRI MBARAWA AFUNGUA BARABARA YA JUU KURAHISISHA SHUGHULI ZA UJENZI

Na Magreth Mbinga

“Leo tupo hapa kuhakikisha tunafungua upande wa pili wa barabara hii ili kuruhusu magari yaweze kupita na hii itakuwa zawadi kubwa kwa Wananchi wa maeneo haya hasa katika kushehereke sikukuu ya mwaka mpya .”

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Prof. Makame Mbarawa katika ufunguzi wa njia ya pili ya barabara ya juu inayojengwa eneo la uhasibu ambapo itasaidia kupunguza foleni na mkandarasi kuweza kuendelea na Ujenzi kwa urahisi.

“Tunaenda kwa awamu Leo tunafungua barabara hii hatua inayofuata tena tutakwenda kufungua daraja la bandari ambalo ni muhimu sana hivi sasa lipo katika hatua za mwisho baada ya hapo tutakwenda kumalizia daraja la Chang’ombe”amesema Prof. Mbarawa.

Pia Prof. Mbarawa amesema wanaamini kama mkataba ulivyosema kwamba barabara hiyo inatakiwa imalizike machi 27,2023 amewahakikishia Watanzania kwamba barabara hiyo itamalizika kwa wakati kama ilivyo ainishwa katika mkataba.

“Barabara hii itamalizika kuanzia mjini mpaka mbagala magari yataenda vizuri lakini kuanzia mbagala kwenda mbele Kuna changamoto kubwa ya magari foleni ni kubwa tayali tumeshafanya usanifu na mwaka 2023 tutaanza kuendeleza kipande Cha Kilometa 17 tutaitanua mpaka Vikindu kwa kufanya hivo hakutakuwa na msongamano tena katika barabara hii”amesema Mhe. Mbarawa.

Aidha Mbunge wa Jimbo la Mbagala Mhe. Abdallah Chaulembo amemshukuru Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwarahisishia usafiri maana barabara hiyo ilikuwa inasumbua takribani miaka 15 .

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha ambazo anazidi kutupatia Wilaya ya Temeke ambapo barabara tunaziona kama hivi “amesema Mhe. Chaulembo.

Sanjari na hayo Meneja wa mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka Jijini Dar es Salaam awamu ya pili Mhandisi Barakaeli Mmari amesema mradi huo unahusisha Ujenzi wa barabara zenye urefu wa km 20.3 ,vituo 27 vya mabasi yaendayo haraka ,barabara za juu 3 pamoja na njia za maji zinazopita chini zenye urefu wa zaidi ya km 40.

“Tunaendela na Ujenzi na mara ya mwisho Mh Waziri ulifika hapa Novemba 15,2022 tulikuwa tumefika 80% sasahivi Ujenzi umefikia 82% mkandarasi akiruhusu magari kupita juu itamsaidia kumalizia Ujenzi vizuri sababu barabara inayojengwa ni yazege na inahitaji siku 27 ili kuruhusu magari kupita”amesema Mhandisi Mmari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!