Home Kitaifa WAZIRI MAVUNDE NA MCHENGERWA KUKUTANA KUSHUGHULIKIA TOZO ZA HALMASHAURI KWENYE MADINI

WAZIRI MAVUNDE NA MCHENGERWA KUKUTANA KUSHUGHULIKIA TOZO ZA HALMASHAURI KWENYE MADINI

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amesema Wizara ya Madini imekubaliana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kukutana na kutatua changamoto ya tozo zinazowekwa na Halmashauri kwa wachimbaji wa madini nchini.

Mavunde ameyasema hayo mkoani Morogoro katika kikao chake wachimbaji wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero zao

Akizungumza Mavunde amesema “nimesikiliza kwa umakini mkubwa kilio hicho cha tozo za Halmashauri na tozo nyinginezo kwa wachimbaji wadogo,kero hizo sio tu kwa wachimbaji wa Morogoro zipo maeneo yote nchini.

Tunayo maelekezo ya Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kwamba Wizara hizi mbili zikutane kushughulikia suala hili,” amesema na kuongeza

Nataka niwahakikishe mimi na Mwenzangu Mh. Mohamed Mchengerwa tumekubaliana mara baada ya ziara ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Morogoro tutaitisha kikao cha pamoja ili kushughulikia suala hilo,” amesema Mavunde

Aidha, amewahakikishia wachimbaji wa Morogoro juu ya dhamira ya Mh. Rais Samia kuongeza nguvu kwenye eneo la Utafiti wa Madini ambapo na mkoa wa Morogoro pia utanufaika.

Mh Mavunde ameipongeza Ofisi ya Madini Mkoa wa Morogoro kwa kuvuka lengo la ukusanyaji maduhuli kufikia Sh Bilioni 4.9 zaidi ya lengo lililowekwa la Sh bilioni 4.2.

Awali, akisoma risala kwa niaba ya wachimbaji, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Morogoro. (MOREMA) Dkt. Omar Mzeru ameshukuru Rais Samia kwa kutoa mashine za uchorongaji kwa wachimbaji wadogo na kutumia fursa hiyo kumuomba Waziri wa Madini kushughulikia changamoto kubwa inayotokana na uwepo wa tozo nyingi zinatozwa na Halmashauri na Taasisi nyingine za serikali kwakuwa zimekuwa zikiwarudisha nyuma kimapato wachimbaji wadogo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!