OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah J. Kairuki akiwasili Makao Makuu ya Ofisi za Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dar es salaam na kupokelewa na Mkurugenzi wa DART, Dkt. Edwin Mhede. Leo tarehe 10 Oktoba 2022
Waziri Kairuki atafanya ziara ya siku mbili katika Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ambapo siku ya kwanza atapokea Taarifa ya utendaji wa DART na kuongea na Menejimenti ya Wakala pamoja na Watumishi wa DART.
Siku ya pili, atatembelea Miradi ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa kukagua vituo vya mabasi na huduma zinazotolewa kuanzia kituo cha Mabasi cha Kimara mpaka Mbagala.