
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo, amemteua Bw. Abdulmalik Mollel kuwa Mjumbe wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Biashara (CBE), kwa mujibu wa Sheria Na. 3 ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya Mwaka 2020.
Taarifa iliyotolewa na Bi. Suzan Clement Mshakangoto, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Viwanda na Biashara, tarehe 18 Machi 2025, inabainisha kuwa Bw. Mollel, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gel Group yenye makao makuu jijini Dar es Salaam, tayari ameshaanza rasmi majukumu yake tangu tarehe 10 Machi 2025.
