Home Kitaifa WAZIRI JAFO AIPONGEZA KADERES KWA KUANZISHA KILIMO CHA MITI YA HEWA UKAA...

WAZIRI JAFO AIPONGEZA KADERES KWA KUANZISHA KILIMO CHA MITI YA HEWA UKAA KAGERA

Na Theophilida Felician Kagera.

Waziri wa Nchi, ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Saidi Jafo ameipongeza kampuni ya Kaderes pamoja na Rabo bank kwakushirikiana pamoja na kuanzisha ulimaji wa miti ya hewa ukaa.

Akitoa pongezi hizo waziri Jafo akiwa amefanya ziara ya kukitembelea kituo kinachotumika kuotesha miche ya miti ya miparachichi kinachoandaliwa na watu hao maeneo ya kata ya Kilimilile wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera amesema kwamba hatua ya Kaderes kuanzisha kilimo mseto chenye miti ya hewa ukaa ni hatua nzuri mno kwani kilimo hicho kitakuwa na faida mbalimbali ikiwemo ya uchumi kwananchi sambamba na utunzaji wa mazingira.

“Kama na vyokumbuka ni kwamba mwaka (2021) Oktoba ofisi yangu ilitoa miongozo yaani muongozo wa hewa ukaa pamoja na kanuni zake za Oktomba (2021) na hivyo tukawataka makampuni mbalimbali sasa yaanze mchakato wa kushirikiana na jamii hasa ya kitanzania katika biashara ya hewa ya ukaa leo hii nimefarijika sana kuona Kaderes na Rabo bank kwakuonyesha utofauti mkubwa wao wamejielekeza katika biashara ya hewa ukaa kwakutumia eneo la kilimo mseto jambo hili ni kubwa halijawahi kutokea Nchini mwetu Tanzania” ameeleza waziri Jafo.

Pia amesema kuwa amefurahishwa na mikakati mikubwa waliyonayo Kaderes na wenzao wa Rabo bank juu ya kuzalisha miche milioni Tano( 5 )kila mwaka malengo amboyo ni makubwa kwani lengo la kila Halmashauri nchini inapaswa kupanda miti miloni 1. 5 kwa mwaka hivyo wao wamevuka mara tatu ya malengo ya wilaya.

Faida za miti ya hewa ya ukaa amezitaja kwamba wakulima wataweza kuuza mazao yao wanayoyazalisha kupitia miti hiyo vile vile wataweza kufanya shughuli za bishara ya hewa ukaa.

Binafsi ni kiwa waziri niliyepata dhama katika eneo hili niwapongeze sana Kaders na Rabo bank kwakazi hii kubwa lakini niupongeze uongozi wa wilaya Misenyi na Mkoa Kagera kwakujipambanua katika eneo hili niwaombe sasa watanzania huu ni mwanga mpya umefunguka kwa watanzania, mwazo wakati tunazungumza haya wengine walijua ni historia tuu au ni hadithi tuu lakini sasa unaona jinsi gani wadau wameingia kazini kufanya kazi kwa vitendo” Waziri Jafo akiendelea kutoa ufafanuzi.

Ameiomba mikoa yote na Halmashauri zote waweze kutoa ushirikiano kwa wadau kama Kaderes kwa malengo ya kujenga uchumi wa nchini huku akisema kwamba anatamani jambo kama hilo liweze kutanuka mikoa yote.

Amesisitiza kuwa ofisi yake itahakikisha inatoa ushirikiano kwa wadau ili malengo ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja sambamba na utunzaji wa mazingira uweze kufikia malengo makubwa yaliyokusudiwa na Serikali katika eneo hilo.

Hata hivyo ametoa wito kwa watalaamu kutoka vyuo vya kilimo nchini kushirikiana vizuri na wadau ili kuendelea kufanya mageuzi makubwa zaidi.

Leonard Kachebonaho ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo akiambatana na wenzake Rabo bank ameeleza kuwa kituo hicho chakuoteshea miche kwa sasa kina miche ya miti karbia laki mbili (2) hivyo kufikia mnamo mwezi wa 9 mwaka huu kitakuwa na miche milioni tano walioipanga kuigawa kwa wakulima watakaokuwa wamesajiliwa kwenye mradi huo wa kilimo mseto ambao unalenga kuewawezesha wakulima kupata pesa mara mbili moja ikiwa ni kupata pesa na kijani ya mkulima ambayo inatokana na shamba alilolilima pili anapata pesa kulingana na matunda aliyoyazalisha.

Ameongeza kuwa miti hiyo inazalishwa kwa kiwango kikubwa cha gharama kwani mbengu zinatolewa Mbeya na miche hiyo wataitoa bule wa wakulima.

Ameishukuru Serikali kwa jinsi inavyotoa ushirikiano wa hali juu kwa wawekezaji hao ambapo amemshukuru waziri Jafo kukubali mwaliko wakufika Kagera na kuwatembelea kujione jitihada zao kiuwekezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!