Home Kitaifa WAZIRI DKT. GWAJIMA: MTOTO ALIYE CHINI YA UMRI WA MIAKA 18 MARUFUKU...

WAZIRI DKT. GWAJIMA: MTOTO ALIYE CHINI YA UMRI WA MIAKA 18 MARUFUKU KUONEKANA KWENYE KUMBI ZA SHEREHE

Na Magreyhy Katengu

Wamiliki wa kumbi za starehe na Washereheshaji (MC) nchini, wametakiwa kuzingatia Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 ili ya kuwataka kutoruhusu mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 kushiriki katia kumbi za sherehe kuanzia saa mbili usiku ili kusadia kupunguza wimbi la mmomonyoko wa maadili kwa watoto.

Tamko hilo limetolewa leo Jijini Dar es salaam na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima walipokutana na wadau hao kufuatia tukio lililotokea hivi karibuni na kusambaa Maudhui katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha watoto wakicheza mziki katika sherehe iliyokuwa ikiendeshwa na Nabi Nsena maarufu kama (MC Nsena) na. kuleta sintofahamu katika jamii.

Waziri Dkt. Gwajima amesema Malezi bora huanzia katika ngazi ya familia lakini pia hata washehereshaji na wamiliki wa kumbi za starehe, wapiga muziki (DJs) na Wazazi wana nafasi kubwa katika kumlinda Mtoto ili kudhibiti mmomonyoko wa maadili dhidi ya watoto kupitia Sheria ya Mtoto, Sura ya 13 kifungu cha 158 cha Katazo la Jumla.

“Pamoja na juhudi zinazofanywa na Wizara kwa kushirikiana na Wadau, bado baadhi ya familia na jamii wakiwemo wazazi na walezi hawatimizi wajibu wao kwa ufanisi kwenye malezi na makuzi stahiki ya watoto kwabi baadhi ya Watoto wanatumiwa kwenye shughuli za sherehe ikiwemo harusi kutoa burudani ya mziki ambapo jambo hilo linaathiri malezi na makuzi yao Matendo hayo yasipodhibitiwa yatachochea mmomonyoko wa maadili na kuwaweka watoto katika hatari ya kufanyiwa ukatili .” Amesisitiza Waziri Dkt. Gwajima

”Nawaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kote kushirikiana na Wadau wa Maendeleo na vyombo vya habari, polisi jamii na madawati ya jinsia ya wanawake na watoto ya Jeshi la Polisi kutekeleza mpango wa elimu kwa jamii kuhusu Sheria ya Mtoto” Ameagiza Waziri.

Sanjari na hayo ametumia nafasi hiyo pia kumuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuunda Kamati mtambuka na kuipa jukumu la kuja na mpango wa haraka, wa muda mfupi na mrefu wa kudhibiti uvunjifu wa Sheria ya Mtoto na Sheria nyingine za nchi zinazohusika na kutunza maadili.

“Natoa siku 21 nipokee yatokanayo na kazi ya Kamati hii ili nitoe mrejesho kwa jamii na kuandaa mjadala wa wazi ili jamii nayo itoe maoni yajumuishwe kwenye kazi ya Kamati kwa ajili ya umiliki wa pamoja kama jamii.” ameagiza Dkt. Gwajima.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Kedmon Mapana amesena Sanaa imebeba wasanii wa aina mbalimbali hivyo muongozo utaandaliwa kuwaongoza wasanii wote hata nyimbo wanazotunga kabla ya kuiachia katika mitandao ya kijamii wasome uwaongoze kwani wadau wa sanaa kusoma na kuzingatia kanuni za Baraza hilo kwani zimefafanua vizuri namna ya kuwalinda watoto dhidi ya maudhui katika kazi zao za sanaa.

”Teknolojia imekuwa sana tofauti na zamani kwani sasa mtu anaweza kukaa nyumbani kwake akatumia simu ya mkononi akairushia Mtandaoni Basata wakistuka ishasambaa ndani ya masaa machache hata akiitwa msanii ili asaidie tayari amesha sambaza YouTube na watu wengi wamesoma hivyo lazima ndani ya siku gizo 21 lazima tukae na TCR na wadau wengine kuweka Muongozo ‘” Amesema Mapana

Naye Mwenyekiti wa Washereheshaji MC Boaz Mwakajumba amesema changamoto ni wazazi na walezi kutumia watoto kwenye kumbi za starehe bila kujali kuwa nyimbo nyingi zinazotungwa sasa zipo kinyume na maadili kwa sababu hazihaririwi kabla ya hazijarushwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!