Home Kitaifa WAZIRI AWESO AKABIDHI MITAMBO NA VIFAA VYA KUCHIMBIA VISIMA VYA MAJI...

WAZIRI AWESO AKABIDHI MITAMBO NA VIFAA VYA KUCHIMBIA VISIMA VYA MAJI KWA DDCA

Na Mercy Maimu

Siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuelekeza kuchimbwa visima kwa haraka katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam ili kuongeza upatikanaji wa maji, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amekabidhi jukumu hilo kwa Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA).

Jukumu hilo limekwenda sambamba na kuwakabidhi mitambo na vifaa vya kisasa vya uchimbaji visima na mabwawa ambavyo vimenunuliwa hivi karibuni na Serikali.

Akizungumza leo Alhamisi Novemba 3, 2022, Waziri Aweso ametoa maelekezo kwa kitengo hicho kwenda kuanza kufanya kazi hiyo kwa haraka kama ambavyo imeelekezwa na Waziri Mkuu.

Amesema maji yaliyo chini ya ardhi ni takribani mita za ujazo 21 bilioni hivyo wakati umefika wakati kugeukia rasilimali hiyo kupata maji ya uhakika.Katika maagizo yake Aweso amewataka DDCA kufufua visima 197 ambavyo vilichimbwa lakini havikufanikiwa kutoa maji, pia ameagiza kuchimbwa kwa visima vipya katika eneo hilo la Kigamboni.

“DDCA kwa sasa hamna kisingizio chochote mnayo ya kisasa inayoweza kufanya kazi hiyo kwa haraka na ufanisi mkubwa. Sasa niwaombe nendeni mkafie site (eneo la mradi)”.

“Naamini timu niliyonayo ni nzuri na tumepewa jukumu la kuhakikisha tunavuka salama katika kipindi hiki cha ukame. Niwaeleze Dawasa kipindi hiki ni cha mpito hamko peke yenu, tunatambua kazi kubwa mnayofanya tutahakikisha tunavuka pamoja,” amesema Aweso.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Dawasa) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema mradi wa maji wa Kigamboni utasaidia kupunguza changamoto iliyopo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!