Na Neema Kandoro, Mwanza
Mwenyekiti wa wazee Mkoani Mwanza Charles Masalakulangwa alisema wanayo imani kubwa na Makonda kwani ana weledi na uzoefu katika ulingo wa siasa.
Wazee hao mkoani Mwanza walimpongeza na walimsimika Makonda kwa jina la Nsumba Ntale ikimainisha Kiongozi Mkuu Kijana kwenye jamii ikiwa kama ishara ya kumtakia Kila kheri katika safari yake ya kisiasa.
Walimuomba aombe kwenye chama tawala wazee kupewa vipaumbele kwenye kupata huduma za afya kwa vile wengi wao hawana nguvu na uwezo wa kupata huduma hiyo kwa wakati.
Naye Mzee Maarufu Edward Maleka amesema uzoefu alionao Makonda kwenye Siasa utaleta mageuzi makubwa kwenye Chama Cha Mapinduzi kwani ni mtu Jasiri anayeweza kukisemea chama hicho bila uwoga.
Alisema ana imani kuwa Makonda ataleta mageuzi makubwa ndani ya chama hicho na hivyo kukiwezesha kupata ushindi mnono dhidi ya vyama vya upinzani.