Home Kitaifa WAZAZI WATAKIWA KUTOWAACHIA USIMAMIZI WA MAADILI WALIMU PEKE YAO

WAZAZI WATAKIWA KUTOWAACHIA USIMAMIZI WA MAADILI WALIMU PEKE YAO

Na Shomari Binda-Musoma

WAZAZi na walezi wametakiwa kutowaachia usimamizi wa malezi ya maadili ya wanafunzi walimu peke yao.

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa Kata ya Mukendo manispaa ya Musoma, Abasi Chamba kwenye maafali ya 8 ya shule ya awali na msingi ya Imam Shafii.

Amesema ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili ambao unaonekana kwa sasa kuwa tishio kwa jamii no vyema usimamizi wake ukawa ni wa kila mmoja.

Amesema usimamizi wa maadili mazuri sio kwa walimu peke yao bali jukumu hilo linapaswa kufanywa kwa ushirikiano na wazazi pamoja na walezi.

Chamba amesema wanafunzi wanapokuwepo shuleni walimu wanakuwa kwenye uangalizi lakini wanaokuwa nyumbani ni jukumu la wazazi na walezi.

Diwani huyo amesema mmomonyoko wa maadili haupaswi kuonekana ukiendelea kwenye jamii na watoto kualibikiwa hivyo lazima kuyasimamia.

“Nashukuru kualikwa kwenye maafali haya ya shule ya Imam Shafii na nimeshuhudia vijana wenye maadili waliofundishwa elimu bora ya dunia na akhera”

“Lakini uko kwenye jamii yetu bado kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili lazima.tukasimamie ili kuwalinda vijana wetu” amesema Chamba.

Kwa upande wake meneja wa shule za Imam Shafii, Yahaya Kange amesema maadili kwenye shule hizo ni suala la kipaumbele na wataendelea kulisimamia.

Amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hasaan inapambana na kusimamia maadili na wao kama shule wanasimamia maadili mazuri.

Wazazi na walezi waliohudhuria maafali hayo wamewapongeza walimu kwa kuwasimamia wanafunzi hadi kuhitimu elimu ya msingi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!