Home Kitaifa WAZAZI WATAKIWA KUFATILIA MIENENDO YA WANAFUNZI WAKATI WA LIKIZO

WAZAZI WATAKIWA KUFATILIA MIENENDO YA WANAFUNZI WAKATI WA LIKIZO

Na Shomari Binda-Musoma

WAZAZI na walezi wametakiwa kufatilia mienendo ya wanafunzi wakiwa nyumbani wakati wa kipindi cha likizo.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa shule ya Siloam pre & preymary school, Winner Alphonce, kabla ya kukabidhi matokeo ya wanafunzi ya mitihani ya kumaliza muhula.

Amesema walimu wamefanya kazi nzuri katika kipindi cha masomo na wakati wa sasa ni wazazi na walezi kuwa nao karibu.

Alphonce amesema muda wa likizo sio nafasi ya kuwaacha wanafunzi kushinda kwenye tv na kufatilia tamthilia na vipindi visivyo na manufaa kwao.

Zaidi ya siku 30 wanafunzi warazokaa nyumbani ni muhimu kujisomea masomo ya ziada ili wakirudi shuleni wasianze upya.

Mkuu huyo wa shule amesema maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo ni mazuri kutokana na matokeo ya mitihani ya hivi karibuni hivyo ni muhimu kuwa na muendelezo.

Tunaenda kwenye kipindi cha likizo tusiwape nafasi wanafunzi kushinda kwenye tv bali wawe na muendelezo wa kusoma”, amesema Alphonce.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Henoko Imani amewataka wazazi wa wanafunzi kuzingatia suala la ulipaji ada kwa wakati ili kutimiza majitaji ya walimu na shule kuongeza ufanisi katika ufundishaji.

Kwa upande wao wazazi na walezi wamesema watazingatia maelekezo ya walimu juu ya wanafunzi katika kipindi chote cha likizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!