Na Magrethy Katengu
Wazazi wameshauriwa kuwajengea watoto Utamaduni wa kusoma vitabu ili viwasadie kuongeza ujuzi kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii ikiwemo kiuchumi,kijamii kisiasa .
Ushauri huo umetolewa leo Dar es salaam na Mkurugenzi mwanzilishi wauzaji wa vitabu vya big bad wolf Mohamed Noor wakati akitoa taarifa juu ya tukio la ufunguzi wa wiki ya uuzaji wa vitabu vya Big Bad Wolf Tanzania katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia 8-18 Septemba mwaka huu ambapo kutakua na punguzo la 80% huku kiingilio likiwa bure hivyo Wazazi ni budi kuja na watoto wao kuwanunulia vitabu wajisomee Ili viwape hamasa ya kuwatambua watu mashuhuri walifanyaje hadi wakafikia vilele vya mafanikio .
“Ni matumaini na Imani yetu kuwa Watanzania watafaifika kwa kiasi kikubwa na vitabu kwani ni kwa ajili ya kila mtu hivyo ni vyema kuja na ndugu,jamaa,kujipatia ujuzi kupitia vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kingereza“amesema Mohamed
Hata hivyo amesema kutakuwa na shindano Maalumu liitwalo book haul contest,ambapo washiriki wanaoshiriki picha/video ya ununuzi wao kwenye Facebook,Instagram,twiter kwa kutumia hashtag#BBWBookHoul Wanaweza kujishindia vocha ya BBW yenye thamani ya TZS 50,000(washindi 10watachaguliwa kila siku) na mshindi mmoja ambaye atabahatika kujishindia tunzo ya toroli la vitabu
Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa vitabu vya Big Bad Wolf Andrew Yap amesema wamefurahishwa kuja nchi Tanzania kuleta Mauzo kwa mara ya kwanza hivyo ni hatua ya kusisimua na Muhimu kwetu katika vitabu tulipoanza safari kupelekea Afrika kuanzisha kama kimbilio letu kujenga dhamira ya kujenga kizazi kipya cha wasomaji vitab
“Kutakuwa na nada 15,000 zinazopatikana na vitabu 500,000 vipya vya Kingereza vinavyotolewa tunataka watanzania kutoka nya nja mbalimbali -wawe vijana au Wazee wagundue furaha ya kusoma na kupata maarifa bila kujali kiwango cha kipato chao“amesema Andrew