Home Kitaifa WAZAZI NA WALEZI WAPELEKENI WATOTO KUSOMA ELIMU YA MUNGU: MTEMVU

WAZAZI NA WALEZI WAPELEKENI WATOTO KUSOMA ELIMU YA MUNGU: MTEMVU

Na Magrethy Katengu

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es salaam Abbas Mtemvu amewaomba Wazazi na Walezi kuhakikisha wanawepeleka watoto kusoma elimu ya Mungu ikiwemo wa dini ya kiislam(Madrasa) ili iwasaidie kutunza maneno ya Mwenyezi Mungu akilini mwao na kuishi wakiwa na maadili mema katika jamii.

Ombi hilo amelitoa jijini Dar Es Salaam katika mashindano ya kwanza ya Kuhifadhi Quran tukufu, yaliyoandaliwa na Al Madrasat Maadu-Diin yaliyofanyika katika ukumbi wa Grand Paradise,Yombo Vituka Jijini humo ambapo amesema watoto wakianza kupata malezi mazuri ya kidini tangu wakiwa wadogo ni faida kubwa sana kwa nchi kujipatia viongozi bora sanaa wa kutegemewa .

Mtemvu amesema Madrasa Ina faida kubwa katika kuwajenga watoto katika misingi bora kiimani huchangia kuwafanya watoto kuwa wampende Mungu na kuhifadhi maandiko yake naye huwapa neema ya baraka kubwa kufanya vizuri katika masomo yao ya darasani .

Mzazi yeyote hujivunia kuona mtoto wake akiwa na tabia njema akipenda ibada na hata elimu ya shuleni kwa kuwa mnaona umuhimu wa Madraasa nawaomba tuungane tuwajali waalimu wanokaa na watoto kuwafundisha kuhifadhi maneno ya Mungu ili nao wapende kazi wanayoifanya ” amesisitiza Abbas

Mtemvu ametolea mfano wake, amesema yeye alikosea mwanzo na alipongundua haraka aliamka na kumpeleka Madrasa akapate mafundisho ya dini hususn Quran ndipo alipoaza kufanya vizuri pia hata Shuleni na kule Marekani anashika nafasi ya pili au ya tatu darasani hivyo ,mafunzo ya Madrasa ni muhimu sana kwa watoto wetu.

Aidha Mtemvu amekipongeza kituo Cha Madrasa Cha Al Madrasat Maadu-Diin kwa kuandaa mashindano hayo ya Quran tukufu kwa Mara ya kwanza ambapo wameonyesha uwezo mkubwa katika uandaaji wake ikiwemo kuyafanya Katika ukumbi wenye hadhi ya juu Jambo ambalo linatoa taswira nzuri kwa kituo hicho katika mashindano yatakayofuata ya Kuhifadhi Qur’aan tukufu.

Hata hivyo amewashauri waumini wa dini ya kiislam na watanzania kwa ujumla kumuombea dua Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika utendaji wake ili Taifa liendelee kupata maendeleo, huku akiwaomba watanzania kuwachangia kwa hali na Mali wahanga wa mafuriko katika Kijiji cha Muhoro kilichopo wilayani Rufiji Mkoani Pwani, ambao nyumba zao zimezingirwa na kujaa maji huku wengine wakiwa wamepoteza makazi yao, kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.

Awali akisoma risala kwa niaba ya kituo Cha Madrasa Cha Al Madrasat Maadu-Diin mlezi wa Madrasa hiyo Bi Hadia Khamis Akida amesema kuwa Madrasa hiyo ilianza ikiwa na wanafunzi wanne pekee lakini Sasa hivi Ina zaidi ya wanafunzi 120 ambao inawalea kiimani na kuwapa mafunzo ya Qur’aan tukufu sambamba na malezi mema hivyo ameongeza kuwa mashindano hayo ambayo yanafanywa na Madrasa hiyo kwa mara ya kwanza yatakuwa yakifanyika kila mwaka.

Amesema kuwa Madrasa hiyo pia imekuwa ikipata changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa umeme wa uhakika kwa ajili ya watoto kusoma Hata nyakati za jioni pamoja na ufinyu wa eneo la madrasa ambapo pia tayari wameshapata eneo lenye thamani ya shilingi milioni thelathini lakini wameshindwa kulinunua eneo hilo kutokana na kukosa fedha hivyo wamemwomba Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam, Abass Mtemvu kuwa Mlezi wa chuo hicho.

Aidha Madraasa hiyo inataraji kutenga siku maalum kwa ajili ya harambee ili kufanikisha manunuzi ya eneo hilo na atakayeongoza ni Mhe Abbas Mtemvu hivyo kila atakayeguswa monyoni mwake anaalikwa kuchangia chochote ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!