Na Boniface Gideon, TANGA
Mustahiki meya wa Jiji la Tanga Abdarahaman Shiloo amewataka Wazazi Kulipa ada kwa wakati pamoja wakuwalinda Watoto wa jinsia zote kutokana na mabadiliko ya Teknolojia yaliyopo hivi Sasa ambayo yanasababisha Watoto kujiingiza kwenye michezo michafu inayovunja Maadili.
Meya Shiloo alitoa wito huo Jana Wakati wa Sherehe za mahafali ya 19 na 15 kwa Taasisi ya Elimu ya Eckernford ambapo waliofanyiwa mahafali hayo ni wahitimu wa Darasa la Saba na Kidato Cha nne,
Shiloo alisema mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yameleta hatari kubwa zaidi kwa Watoto wa jinsia zote ambapo kwasasa Ulinzi unahitajika zaidi,
“Tulizoea kumlinda Mtoto wa Kike peke yake lakini kwasasa tunalazimika kuwalinda wote wawili hivyo niwaombe Wazazi, walezi na Jamii kwa ujumla tuubebe huu msalaba ili kunusuru vizazi vyetu” Alisema Shiloo
Aliwataka Wazazi na Walezi kujenga Utamaduni wakukagua kazi za Watoto wanaporejea kutoka Shule ili kufahamu Maendeleo na mahudhurio ya Watoto,
“Hebu tujenge desturi zakupitia kazi za Watoto wetu wakitoka Shuleni, hii itatusaidia kufahamu Maendeleo ya Mtoto pamoja na mahudhurio yake Mana Unaweza ukasema Mtoto kaenda Shule kumbe yupo Mtaani tu “ Alisisitiza Shiloo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Daniel Tarimo alisema Taasisi hiyo inamiaka zaidi ya 24 tokea kuanzishwa kwake na imekuwa ikizingatia Maadili ya Dini zote,
“Taasisi yetu inazingatia Maadili ya Dini zote na tunawalea kwakufuata Misingi ya kidini ili kutengeneza Taifa lenye Misingi imara ya Maadili mema” Alisisitiza Daniel
Alisema changamoto kubwa zinazowakabili ni Wazazi na Walezi kutokulipa ada ya Shule kwa Wakazi pamoja na kutokuwa Karibu na Watoto wao,
“Changamoto kubwa tuliyonayo hapa ni Wazazi na Walezi kutokulipa ada kwa wakati,ada hizi ndizo zinazoendesha Shule kwenye kila idara , hivyo niwaombe Wazazi na Walezi wajitahidi kulipa kwa wakati pamoja na kuwa Karibu na Watoto” Alisisitiza
Kwaupande wake Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga INSP Tatu Kibwende Alisema suala malezi sio jukumu la mzazi pekee yake Bali linahusisha Jamii nzima kwa ujumla,
“Suala la Malezi ya Watoto wetu linahusisha Jamii nzima kwa ujumla na sio watu wachache hivyo niwaombe Wazazi na Walezi tuwe Karibu na Watoto wetu ili tufahamu mienendo ya tabia zao” Alisema Tatu
Mwisho