Home Kitaifa WAWILI WASHIRIKILIWA NA POLISI KWA KULAGHAI

WAWILI WASHIRIKILIWA NA POLISI KWA KULAGHAI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashilia watu wawili akiwemo Emanuel Paul Karata (35) mchungaji wa kanisa la
PENTEKOSTE GOSPEL MISSION lililopo kibaha kwa ulaghai wa kutaka kupata waumini kwa kusingizia mchawi amedondoka kwenye maombi ya mkesha wake na waumini.

Wamewashikilia kwa mahojiano kutokana na taarifa za mtu mmoja jinsia ya kiuume Basenga Silvester Matheo (59) kudondoka kanisani akiwa anasafiri kwa ungo wa kichawi au kishirikina.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini Kibaha mkoani Pwani Kamanda wa Polisi ACP Pius Lutumo amesema tarehe 24 mwezi huu majira ya saa 09:00hrs huko katika kituo cha polisi kibaha mkoa wa pwani alitoa taarifa za mtu mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Basenga Silvester Matheo (59) mkazi wa miswe wilaya ya kibaha akiwa amesafiri kwa ungo wa kishirikina na kudondoka kanisani hapo na kuleta taharuki kubwa kwa waumini.

Katika uchunguzi, Jeshi la Polisi lilibaini kuwa tukio hilo ni tukio la kutengeneza kwa lengo la kuwalaghai au kuwahadaa waumini na wananchi kwa ujumla kwa lengo la kupata waumini zaidi na kujipatia kipato.

Ilielezwa kwamba siku ya tukio kulikuwa na ibaada ya mkesha ambapo mtuhumiwa akiwa na wenzake sita alidondoshwa kwa sala za maombi ya waumini na mchungaji wao na wenzake wakafanikiwa kutoroka kichawi“.

ili kuthibiti taharuki hiyo mchungaji alimchukua mtu huyo na vifaa vyake vya kishirikina na kumuweka
ofisini kwake hadi asubuhi polisi walipofika na kumchukua”

Bwana BUSENGAS/OSILVESTER MATHEO alijinisibu kuwa yeye na wenzake walifika kanisani hapo kishirikina kwa lengo la kupima Imani ya waumini
hao kwa mwenyezi mungu.

Aidha mtuhumiwa aliahidiwa kulipwa Tsh. 50,000/= baada ya kutimiza lengo lao la kilaghai.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa onyo na tahadhari kwa watu wenye tamaa ya
kupata kipato cha haraka kwa kufanya ulaghai kuacha mara moja.

Aidha Jeshi la Polisi linatoa wito kwa waumini kuwa makini na watu wachache wanaotaka kuharibu Imani za kidini kwa tamaa ya kipato.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!